HEADER AD

HEADER AD

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI NA MEGA WE CARE WAANDAA KAMBI YA KUPIMA HOMA YA INI


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Kampuni ya Dawa ya Mega We Care inaendelea na maandalizi ya kambi ya Uchunguzi wa homa ya Ini kuelekea maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani, Julai 28, 2026.

Kambi hiyo inatarajiwa kufanyika katika Kituo cha Kliniki ya Muhimbili Sokoine Drive Medical Centre (MNHSDMC) kilichopo mkabala na SGR jijini Dar es Salaam. 

Ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwafikia Wananchi na kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kupima homa ya Ini mapema pamoja na kupata matibabu.

Katika ushirikiano huo, Mega We Care imetoa mchango wa Dawa na Vifaa Tiba vingine vya kitabibu vitakavyotumika kutoa huduma wakati wa kambi hiyo. 

Mchango huo ni sehemu ya jukumu la sekta binafsi katika kuunga mkono jitihada za kuboresha afya kwa jamii.

Akizungumzia ushiriki huo, Afisa Habari wa Mega We Care, Bw. Mengi Ntasimba amesema kampuni hiyo imeamua kushiriki kama sehemu ya kurudisha kwa jamii na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.

Siku ya Homa ya Ini Duniani huadhimishwa kila tarehe Julai 28. Maadhimisho hayo yanalenga kuongeza uelewa kuhusu ugonjwa huo, umuhimu wa uchunguzi, kinga na upatikanaji wa huduma kwa wakati ili kupunguza maambukizi na vifo vinavyotokana na homa ya ini.


No comments