HEADER AD

HEADER AD

MADINI YENYE THAMANI YA BILIONI 3.3 YAKAMATWA

 


Na Alodia Dominick,  Bukoba

MADINI yenye thamani ya Tsh. Bilioni 3.3 yamekamatwa wakati yakitoroshwa katika maeneo mbalimbali kwa kipindi cha Julai 2025 hadi Machi 2026 huku madini yenye thamani ya Tsh. Bilioni 1.6 yakikamatwa mkoani Kagera kwa kipindi cha Juni hadi Julai 2026.

Hayo yamebainishwa Julai 13, 2026 na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa akiwa katika ziara mkoani Kagera kwa lengo la kutoa tamko la serikali kuhusu matukio ya utoroshaji wa madini ya dhahabu na vito yaliyokamatwa hivi karibuni mkoani humo.

            Naibu Waziri wa madini Dkt. Steven Kiruswa akiwa mkoani Kagera akizumgumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali nchini juu ya utoroshaji madini na tamko la Serikali.

Akitoa taarifa ya utoroshaji wa madini Dkt Kiruswa ameeleza kuwa, kwa kipindi cha Julai 2025 hadi Machi 2026 madini yenye thamani ya Sh. Bilioni 3.3 yalikamaatwa wakati yakitoroshwa katika matukio 55 maeneo mbalimbali hapa nchini.

Akizungumzia madini ambayo yamekamatwa mkoani Kagera amesema kuwa, Juni 29, 2026 ilifanyika oparasheni katika eneo la Benako wilaya ya Ngara na  katika oparasheni hiyo polisi walibaini na kukamata viroba 20 vya madini ya vito sawa na kilo 627.2 yenye thamani ya  Tsh. Milioni . 10.9 na kodi ya serikari Tsh. Milioni 1.


"Watuhumiwa walikuwa wanne mmoja wao ambaye ni Petro Michael Kihiga akiwa na leseni ya udalali namba DL0266LMD/aloyoipata Mei 25, 2026 mkoani Lindi na kupewa kibali cha kusafirisha madini yenye gramu 273 huku uzito halisi uliokamatwa ulikuwa ni kilo 627.2. Kwa kutumia kanuni za madini (ufililishaji wa makosa) za mwaka 2022 mtuhumiwa alikiri makosa na kulipa faini" amesema Dkt. Kiruswa.

Aidha Julai mosi 2026 askari walikamata mtuhumiwa mwingine aliyekuwa amepakiwa kwenye gari la internationalTransit (IT)akiwa na dhahabu yenye uzito wa gramu 4434.66 yenye thamani ya Tsh Bilioni 1.3 na kodi za serikali Tsh. Milioni 125.8  katika eneo la Benako ulipo mpaka wa kwenda nchini Rwanda.

      Aliyesimama katikati ni ofisa madini mkoa wa Kagera Norbert John akionyesha madini aina ya Vito kulia kwake ni mkuu wa wilaya Bukoba Erasto Sima.

"Wakati huo huo Julai 04, 2026 alikamatwa mshirika wa mtuhumiwa wa madini ya dhahabu akiwa na gramu 453 za dhahabu yenye thàmani ya Tsh Milioni 144.2 na kodi za serikali Tsh. Milioni  12.6 " amesema Dkt Kiruswa

Watuhumiwa wa madini ya dhahabu wamefikishwa mahakamani na kesi yao iko katika hatua za kutajwa na kutokana na maswala ya kiupelelezi hawajatajwa majina wala mahakama walipofikishwa.

         Aliyesimama katikati ni ofisa madini mkoa wa Kagera Norbert John akionyesha madini aina ya Vito kulia kwake ni mkuu wa wilaya Bukoba Erasto Sima.

Mmoja wa wananchi Christofa Laurian akizungumza na Mwananchi amesema, hatua ya kukamatwa kwa watoroshaji wa madini ni hatua nzuri ambayo inaonyesha kuwa serkali iko makini kufuatilia raslimali za nchi.

Naye Alisia Rwezaura ameeleza kuwa, utoroshaji wa madini ni jambo linalosababisha kupotea kwa mapato ya nchi hivyo watuhumiwa wanapokamatwa na ushahidi wachukuliwe hatua kali za kisheria ili liwe fundisho watu wasiendelee kufanya makosa kama hayo.



No comments