MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI TAIFA AMPONGEZA MKURUGENZI WA HALMASHAURI KWA KUCHAPA KAZI

Na Gustaphu Haule , Pwani
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Fadhili Maganya ( MCC)amemshushia pongezi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dkt.Rogers Shemwelekwa kwa kazi kubwa na nzuri anazozifanya ndani ya Halmashauri hiyo.
Maganya amesema Mkurugenzi huyo tayari ameshavuka hatua moja kwenda hatua nyingine kwakuwa ameonyesha dhahiri namna ambavyo anajitoa na kuwatumikia Wananchi wa Kibaha kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa akizungumza na wanaCCM katika mkutano wake wa ndani uliofanyika Julai 27/2026 katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere."Mnyonge , mnyonge haki yake mpeni huyu Mkurugenzi kwakweli amenikosha sana kwa namna ambavyo anafanyakazi nimeona mengi ni mazuri na yenye faida kwa Serikali na Wananchi wa Manispaa ya Kibaha ", amesema Maganya.
Maganya amefikia hatua hiyo katika mkutano wa ndani wa chama uliofanyika Julai 27/2026 katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu cha Mwalimu Nyerere mara baada ya kumuuliza Mkurugenzi huyo kuhusu suala la fedha za mikopo ya asilimia 10 kwa Vijana,Wanawake na Watu wenye Walemavu na kisha kumpa nafasi Mkurugenzi kueleza namna Halmashauri yake ilivyotekeleza jambo hilo.
Dkt .Shemwelekwa baada ya kupata nafasi hiyo ameeleza kuwa katika Manispaa ya Kibaha hadi sasa wametoa mikopo inayofikia zaidi ya Sh.bilioni 2.1 kwa vikundi 400 na hivyo kuweza kuwafikia zaidi ya wajasiriamali 3000.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dkt.Rogers Shemwelekwa akizungumza mbele ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Fadhil Maganya katika mkutano wa ndani uliofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere Julai 27/2026Amesema pamoja na kutoa mikopo kwa vikundi hivyo lakini bado Halmashauri inajipanga kuendelea kutoa tena mikopo hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 ili kuhakikisha wajasiriamali wengi wa Manispaa ya Kibaha wananufaika na fursa hiyo.
Shemwelekwa amemueleza Mjumbe wa Kamati Kuu huyo kuwa kabla ya kutoa mikopo hiyo yeye binafsi alipita katika kila Mitaa na kila Kata kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi na wajasiriamali namna ya kuomba mikopo hiyo jambo ambalo lilipelekea wajasiriamali wengi kujitokeza na kupata mikopo hiyo.
Amesema awali wengi wao walikuwa wanakopa lakini walikuwa wanashindwa kurejesha hali ambayo ilikuwa inapelekea Serikali kupata hasara ya fedha kupotea lakini sasa hivi fedha zinakopwa na zinarudishwa vizuri.
Dkt.Shemwelekwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kurejesha mikopo hiyo ambayo kwasasa imekuwa na msaada mkubwa kwa Wananchi na wajasiriamali.
Zahanati ya Kilimahewa Kata ya Tangini iliyotembelewa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Fadhil Maganya Julai 27/2026.
Baada ya majibu ya Mkurugenzi huyo ,Maganya ,alieleza kufurahishwa na Mkurugenzi huyo akisema alichokifanya ndicho kinatakiwa kufanywa katika Halmashauri zote nchini na kwamba anampongeza kwa namna ambavyo amejitoa kusaidia Wananchi.
Maganya ameongeza kuwa, amefanya ziara katika Mikoa, Wilaya na Halmashauri nyingi hapa nchini na amekutana na malalamiko mengi kuhusu suala la utoaji wa fedha za mikopo ya asilimia 10 na Kibaya zaidi maeneo mengine fedha hizo hawatoi kabisa lakini kwa Kibaha na Mkurugenzi huyo hakika kazi nzuri sana na inapaswa kuigwa na Halmashauri nyingine.
Pamoja na pongezi hizo lakini pia Maganya amemuagiza Mkurugenzi huyo kuendelea kufanya vizuri zaidi kwa kuhakikisha anashuka chini zaidi katika ngazi ya Mitaa ili kuhakikisha anawafikia watu wengi zaidi wakupata mikopo hiyo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa akizungumza na wanaCCM katika mkutano wake wa ndani uliofanyika Julai 27/2026 katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere.Amesema hataki kusikia suala la Katiba kuwa kikwazo cha wajasiriamali kukosa mikopo na badala yake Mkurugenzi atume wataalam wake ambao watakwenda katika Mitaa kwa ajili ya kuwasaidia wajasiriamali kuandika Katiba hizo.
"Kwa Kweli Mkurugenzi umefanya vizuri sana hata nilipopita katika mradi wa Zahanati pale Tangini nimekuta mambo mazuri na nilikupongeza lakini katika hili la Mikopo nakupongeza zaidi na sasa nataka ushuke chini zaidi katika Mitaa ukawape elimu wajasiriamali," amesema Maganya.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia Kibaha Mjini kuwa Manispaa na sasa Kibaha imekuwa na mafanikio makubwa na hata mapato yameongezeka.
Koka amesema kuwa Manispaa ya Kibaha imeongeza mapato baada ya Rais Samia kuwaleta watendaji wazuri wakusimamia ukusanyaji wa mapato akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dkt.Rogers Shemwelekwa .
"Mwaka 2020 mapato yalikuwa Sh.bilioni 5 lakini mara baada ya kuja watendaji wazuri hasa Mkurugenzi huyu mapato sasa hivi yamefikia Sh.bilioni 26 na uenda yakaongezeka zaidi kutokana na utendaji mzuri wa Mkurugenzi wetu ," amesema Koka.
Hata hivyo,Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibaha Moses Magogwa amesema kuwa Kibaha ipo shwari na Wananchi wanaendelea kufanya shughuli zao za kimaendeleo kama kawaida.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibaha Moses Magogwa.Magogwa amesema kuwa Manispaa ya Kibaha inakua kwa kasi kutokana na uwekezaji wa viwanda ambapo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha kwa uwekezaji mzuri uliofanywa.
Hata hivyo,Magogwa amesema Manispaa ya Kibaha inafanya vizuri katika sekta zote huku akisema kwa upande wa sekta ya elimu inafanya vizuri zaidi kutokana na mfumo wa live teaching uliofungwa na Mkurugenzi huyo kwa zaidi ya Shule Saba.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Fadhil Maganya kushoto pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dkt.Rogers Shemwelekwa (kushoto).katika ziara iliyofanyika Julai 27/2026.





Post a Comment