HEADER AD

HEADER AD

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU AGAWA MITUNGI YA GESI KWA MAMA NA BABA LISHE


Na Alodia Dominick, Bukoba

KATIKA kuunga juhudi za matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini, kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Wazo Mwang'onda amegawa mitungi midogo ya gesi ya kilo 6 kwa Mama Lishe na Baba Lishe Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Mitungi hiyo imegawiwa Augosti 31,2026 na kiongozi huyo ikiwa ni kuunga juhudi za Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan za matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Mwang'onda akiwa shule ya sekondari Kagemu amekagua na kuzindua mradi wa mitungi ya gesi ambayo inatumiwa na shule hiyo kwa ajili ya mapishi shuleni hapo na kugawa mitungi midogo kwa mama lishe na baba lishe ikiwemo kuzindua club ya wapinga rushwa.

Aidha, Mwang'onda amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kinara wa kampeni hiyo na kumpongeza Mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Sima na Mkuu wa shule ya Kagemu kwa kuunga mkono kampeni ya Rais.

       Mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Sima akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa mkuu waa wilaya ya Muleba Abel Nyamuhanga.

"Nawashukuru wananchi kwa kuendelea kuunga juhudi katika harakati za utunzaji wa mazingira kwa kutumia nishati safi ya kupikia katika taasisi zenye watu zaidi ya 100 na matumizi ya majumbani" amesema Mwang'onda

Aidha, amesema gharama za mitungi ya gesi ziko juu ikilinganishwa na uhalisia wake hivyo uongozi wa shule ya sekondari  Kagemu uwasiliane na kampuni ya Olex makao makuu ili waweze kupunguza gharama hizo.

          Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Wazo Mwang'onda akikabidhi mitungi ya gass kwa mama lishe na baba lishe manispaa ya Bukoba.

Mkuu wa shule ya Kagemu Shukuru Dauson  akisoma taarifa ya shule amesema, mradi wa gesi shuleni hapo umegharimu sh milioni tano.

Amesema, gharama hizo zinajumuisha usafirishaji, ununuzi wa mitungi na ujenzi wa eneo la kutunzia mitungi hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Sima amesema, mwenge wa uhuru ukiwa Manispaa ya Bukoba umezindua, kukagua, kutembelea na kuweka mawe ya msingi katika miradi saba yenye thamani ya zaidi ya  Tsh. Milioni 900.

    Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Wazo Mwang'onda akikabidhi mitungi ya gass kwa mama lishe na baba lishe manispaa ya Bukoba.

Aidha miradi hiyo ni pamoja na kituo janja cha kusambaza maji Kabare ka Ngaiza katika shule ya msingi Ibura na sekondari ya Erasto, mradi wa nishati safi ya kupikia na club ya wapinga rushwa shule ya sekondari Kagemu, vyumba viwili vya madarasa sekondari ya Kibeta, zahanati ya Hamugembe, ofisi ya mtaa pwani, mradi wa vijana Kashai na kijana mbunifu Kashai.

        Mmoja wa wakimbiza mwenge wa uhuru akitumia nishati safi ya kupikia ya gess katika shule ya sekondari Kagemu manispaa ya Bukoba.

No comments