MADIWANI NYASA WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA KIBAHA
Na Gustaphu Haule, Pwani
MADIWANI na wakuu wa divisheni kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma wamefanya ziara ya mafunzo katika Manispaa ya Kibaha kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali ikiwemo ukusanyaji wa mapato na kusimamia miradi ya maendeleo.
Ziara ya madiwani hao imefanyika Septemba 28 /2026 ikiongozwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Stewart Nombo huku upande wa Manispaa ya Kibaha wakiwa na mwenyeji wao ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha Dkt.Rogers Shemwelekwa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, Stewart Nombo amesema anaishukuru Manispaa ya Kibaha kwa ukarimu na namna wanavyosimamia miradi yao kwa ushirikiano kati ya wataalamu ,wakuu wa divisheni na madiwani.
Madiwani na Wakuu wa divisheni wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa wakitembelea Shule ya mchepuo wa kiingereza ya Julius Nyerere iliyopo Kata ya Sofu Manispaa ya Kibaha.Amesema,ziara hiyo imewapa ubunifu na namna bora ya Halmashauri yao kuweza kujiendesha, hivyo amemuomba Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha Dkt. Rogers Shemwelekwa kuendelea kushirikiana katika kusukuma gurudumu la maendeleo katika Halmashauri hizo.
Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Khalid Khalif ameipongeza menejimenti na Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kibaha katika kusimamia ukusanyaji na matumizi ya mapato.
Pia,Khalif ameipongeza Manispaa ya Kibaha katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo imekua dhana ya utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa wakitembelea mradi wa karakana ya magari katika kituo cha biashara ATN kilichopo Kata ya Picha ya Ndege.Amesema ziara hiyo ni sehemu ya kujifunza kutoka kwa Halmashauri nyingine ambazo zimefanikiwa hususani katika eneo la ukusanyaji na matumizi sahihi ya mapato kwa ajili ya maendeleo.
"Tumefika Kibaha kwa lengo la kujifunza na kuona kwa vitendo namna wenzetu walivyofanikiwa katika ukusanyaji wa mapato na namna ambavyo wamekuwa wakipiga hatua katika utekelezaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo,"amesema Khalif.
Akizungumza na madiwani na wakuu wa divisheni, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha Dkt. Rogers Shemwelekwa amesema Manispaa ya Kibaha imeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato na utekelezaji wa matumizi katika miradi ya Maendeleo.
Madiwani na Wakuu wa divisheni kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa wakitembelea mradi wa soko la kisasa la Kibiashara Kibaha Shopping Mall lililopo latika Manispaa ya Kibaha.Kuhusu namna Manispaa inavyojiendesha, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha Dkt .Rogers Shemwelekwa amesema madiwani wamekuwa wakishirikiana na uongozi katika kusimamia ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha zoezi hilo linafanyika bila kuhujumu.
Dkt.Shemwelekwa amesema Manispaa ya Kibaha imekuwa ikifanya vizuri na kuwa kinara katika ukusanyaji wa mapato ambapo mwaka 2024/2025 imeshika nafasi ya kwanza kitaifa na 205/2026 ikishika nafasi ya pili na imeendelea kufanya vizuri na hadi Septemba wamefikia asilimia 41.
“Kwa kipindi cha miaka miwili tumefanya miradi mikubwa mingi kutokana na ukusanyaji mzuri wa mapato ya ndani mfano Julai na Agosti pekee tumepeleka Sh.billion 2.6 katika ngazi za kata, na sisi huwa miradi yetu ya mapato ya ndani huisha mwezi wa pili”amesema Dkt. Shemwelekwa.
Hata hivyo ziara hiyo ya madiwani imefanyika katika miradi ya kimkakati ikiwemo mradi wa maegesho ya magari Misugusugu uliopo Kata ya Misugusugu,Mradi wa kituo cha kibiashara Kongowe Kata ya Kongowe, mradi wa kituo cha biashara ATN katika Kata ya Picha ya Ndege,Shule ya Msingi ya mchepuo wa Kiingereza Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kata ya Sofu na mradi wa biashara wa maduka Kibaha Shopping Mall.
Madiwani na Wakuu wa divisheni kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa wakitembelea mradi wa soko la kisasa la Kibiashara Kibaha Shopping Mall lililopo latika Manispaa ya Kibaha.



Post a Comment