HEADER AD

HEADER AD

MWIMBAJI MIRIAM CHIRWA ATINGA TARIME KAMBI LA WATU WENYE ULEMAVU SDA JIMBO LA MARA KASKAZINI


MWIMBAJI wa Injili wa Kanisa la Waadventista Wasabato , Miriam Thomas Chiwa amewaomba wadau wa maendeleo kuwasaidia watu wenye ulemavu wa viungo ili waweze kutimiza ndoto zao waweze kujiinua kiuchumi.

Miriam ameyasema hayo wakati akizungumza na DIMA Online katika viwanja vya chuo cha Mwera Vision  ambapo makambi ya watu wenye ulemavu wa viungo kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Mara Kaskazini linaendelea.

" Nawaomba Mungu awasaidie wadau wafanye pale ambapo wanaweza kusaidia watu wenye uhitaji maalum ili waweze kufanikisha ndoto zao " amesema Miriam.

Ameushukuru uongozi wa North Mara Field pamoja na watu wenye ulemavu katika Jimbo hilo kumwalika kwa ajili ya uimbaji .

     Mwimbaji wa Injili wa Kanisa la Waadventista Wasabato , Miriam Thomas Chiwa.

" Nawashukuru uongozi wa North Mara kwa kunialika kuja kwenye haya makambi bila kumsahau mratibu wa watu wenye ulemavu kanisa la Nyamongo kati Bhoke Orindo kwa kunialika.

" Namshukuru mme wangu Reoben kwa kuniruhusu kuja huku Tarime maana sisi tunaishi Igunga mkoani Tabora. 

" Nawashukuru wazazi wangu kwa malezi bora wamenilea vizuri bila kunibagua wala kuninyanyapaa" amesema Miriam.

Miriam anawakaribisha watu wote wenye ulemavu wa viungo, waumini na wadau mbalimbali kwenye ibada ya kuhitimisha kambi la watu wenye ulemavu Jimbo la Mara Kaskazini siku ya jumamosi( kesho) katika viwanja vya Mwera Vision.

Miriam amesema ibada ni muhimu ni mapatano ya mtu na Mungu huku akiwahimiza watu wenye ulemavu wa viungo kumwabudu na kutumikia Mungu.


No comments