WANAFUNZI 400 MEATU WAPEWA BAISKELI , 82 WADHAMINIWA ELIMU YA JUU

Na Mwandishi wetu, Meatu
Taasisi ya Uhifadhi ya Friedkin Conservation Fund(FCF) kwa kushirikiana na kampuni ya Uhifadhi na Utalii ya Mwiba Holdings Ltd wametoa baiskeli 400 kuwasaidia wanafunzi wa sekondari kufika shuleni kwa wakati.
Baiskeli hizo.zimetolewa kwa Wanafunzi wa vijiji vya Ming’ongwa, Butuli, Bulyandulu, na Mwangudo wanaosoma katika shule za sekondari za Busangwa, Paji, na Mwangudo wilaya ya Meatu,mkoa wa Simiyu.
Akitoa taarifa za miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Friedkin na Mwiba Holdings wilaya ya Meatu,Afisa Miradi kitengo cha ufugaji nyuki wa Friedkin,Baraka Mabula jana September 17,2026 Jukwaa la Mashirika Yasiyo ya Serikali (AZAKI) la Wilaya ya Meatu, amesema Mradi huo wa Baiskeli ulianza mwaka 2023 na unaendelea hadi sasa.
Mabula amesema jumla ya wanafunzi 400 (Wavulana 188 na Wasichana 212) wamepatiwa baiskeli na wamekuwa wakifanyiwa ukarabati wa mara kwa mara ili kuendelea kuzitumia Baiskeli hizo.
"Mradi huu licha ya kusaidia wanafunzi hasa ambao wanaoshi mbali na shule na maeneo yao kuna wanyamapori lakini pia unalengo kuinua viwango vya ufaulu katika wilaya hiyo.
Anasema Baiskeli hizo kwa sasa wanafunzo wanapomaliza kidato cha nne wanazirudisha shule na wanapewa wengine kila mwaka.
Mabula pia alieleza kuwa pia wamekuwa wakitoa Ufadhili wa Masomo wa Friedkin (Friedkin Scholarship Award)kwa Vyuo Vikuu, Vyuo vya Kati, na Kidato cha 5 na 6 (A-Level).
Anasema hadi kufikia Mwaka 2026 Wanafunzi 82 (Wavulana 50 na Wasichana 32) katika ngazi tofauti wamepata ufadhili.
Akizungumzia miradi hiyo,Kaimu Mkurugenzi halmashauri ya Meatu,Protas Dibogo alipongeza Mwiba na Friedkin kwa mchango wao katika elimu na jamii.
"Halmashauri ya Meatu tutaendelea kuwaunga mkono wawekezaji wetu na asasi za kiraia zote ili mtimize malengo yenu"alisema .
Naye Mbunge wa jimbo la Kisesa Musa Godfrey Mbuga alipongeza Friedkin na Mwiba kwa misaada yao lakini akaomba kupanuliwa dilisha na udhamini wa wanafunzi.
Mwiba Holdings Ltd (MHL) ilianza uwekezaji wake wa utalii wa miaka thelathini katika Pori Tengefu la Makao Mwiba baada ya kuundwa kwake mwaka 2008.
Kuanzia Januari 2024, MHL ilipanua shughuli zake katika Pori la Akiba la Maswa baada ya kupata mkataba wa miaka 20 na TAWA kufanya biashara ya utalii.



Post a Comment