ALIYESOTEA FIDIA KWA MIAKA 17 ALIPWA MILIONI 500
Na Dinna Maningo,Tarime
KAMPUNI ya Uchimbaji wa Dhahabu ya Barrick North Mara imemlipa fidia ya Ardhi kiasi cha Tsh. Milioni 500 Augustino Nestory Sasi mkazi wa Nyamongo wilayani Tarime mkoa wa Mara baada ya kushinda kesi ya madai katika Mahakama Kuu Kanda ya Musoma dhidhi ya Mgodi wa North Mara kesi aliyoifungua tangu mwaka 2005.
Akizungumza na Mwandishi wa Habari Augustino amesema kuwa mwaka 2004 akiwa jela gereza la Butimba Mwanza alikokuwa akitumikia kifungo cha miaka 30 jela alijitokeza mtu mmoja ambaye hakumtaja jina akachukua eneo lake lililojengwa uwanja wa ndege wa mgodi wa North Mara, nakusema kuwa
ni eneo lake lililokuwa na viwanja vinne vyote na mgodi ukamlipa fidia huyo mtu ili kupisha ujenzi wa uwanja wa ndege.
ni eneo lake lililokuwa na viwanja vinne vyote na mgodi ukamlipa fidia huyo mtu ili kupisha ujenzi wa uwanja wa ndege.
"Nilitumikia kifungo miaka minne 2004 nikaachiwa huru baada ya kushinda rufaa, kesi ambayo nilishtakiwa kwa hila tu lengo lao likiwa niwekwe ndani wapate mwanya wakuchukua ardhi yangu.
"Nilihukumiwa jela miaka 30 nikatoka Novemba 2004 nilishinda baada ya kesi yangu kusimamiwa na aliyekuwa Wakili wangu Tundu Lissu ninamshukuru sana Lisu bila yeye ningetumikia miaka 30 gerezani.2005 nilifungua kesi ya madai nikashinda, mgodi ulikata rufaa kesi ikaendelea nao ukashinda.
Alisema kuwa 2021alikata Rufaa Mahakama Kuu ya Kanda na alishinda kesi, baada ya kushinda walifanya mazungumzo na mgodi na hivyo kumlipa fidia Milioni 500.
"Nawashukuru mawakili ambao wamesimamia kesi yangu ya madai mpaka nimeshinda kesi niliyoisotea kwa miaka 17, namshukuru Willem Jacobs wa Barrick kwa kusikiliza kilio changu na wamenimelipa fidia" alisema Augustino Sasi.
Augustino aliipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu kuwa kwenye uongozi wake haki yake imepatikana na mgodi umemlipa fidia, kwani tangu 2005 alipofungua kesi yake ya madai ya fidia ya ardhi dhidi ya Mgodi wa North Mara hakuweza kulipwa.
"Serikali zilizopita wakiwemo baadhi ya viongozi wa Serikali ya Tarime na Chama cha Mapinduzi walichochea nisilipwe fidia kuwa mimi ni mwanachama wa CHADEMA wakawa wananiambia kuwa ningekuwa CCM ningelipwa fidia, uongozi wa rais Samia hauna ubaguzi wa vyama" alisema Augustino Sasi.
Post a Comment