GWIBOHA: VIJANA CHANGAMKIENI FURSA KILIMO CHA MBOGA KINALIPA
Dinna Maningo, Tarime
AFISA Kilimo wa Halmshauri ya wilaya ya Tarime Sylvanus Gwiboha amesema kuwa wilaya ya Tarime mkoani Mara bado inategemea mboga toka nje ya wilaya licha yakuwa na misimu miwili kwa mwaka na kwamba hali hiyo inatokana na uzalishaji mdogo ikilinganishwa na mahitaji.
Akizungumza na Dima Online,Gwiboha alizitaja mboga hizo ambazo zimekuwa zikinunuliwa toka nje ya wilaya ya Tarime licha ya wilaya hiyo kuwa na ardhi yenye rutuba inayostawisha kilimo cha mboga.
"Tuna misimu miwili kwa mwaka lakini uzalishaji wa mboga ni kidogo tuna rutuba nzuri ya kulima mboga kama Nyanya, Vitunguu, Kabeji, Sukumawiki na zinginezo, niwaombe wananchi watumie fursa hiyo ili washindane na bidhaa toka Kirumi, Kyabakari, Bunda, Lamadi, Magu na mwanza,kilimo hiki cha mboga kinalipa naomba vijana watumie fursa hii kujipatia kipato"alisema Gwiboha.
Pia Gwiboha alisisitiza umuhimu wa maandalizi ya kitalu,alisema kuwa maandalizi mazuri ya kitalu cha mboga hutoa miche bora tayari kwa kupandwa katika shamba kuu na kwamba mavuno mazuri huanzia maandalizi kwenye kitalu.
"Unaweza kuwa na mbegu bora lakini kama maandalizi ya kitalu sio mazuri utaishia kupata mavuno hafifu.Kauli mbiu inasema " Lima Mboga uboreshe lishe na kipato cha familia/kaya" kuna fursa kubwa katika kilimo cha mboga kijana changamkia fursa mavuno utapata baada ya miezi mitatu au minne tangu ulipopanda"alisema Gwiboha.
Post a Comment