MWENYEKITI WAZAZI KUTUMIA SHERIA,KANUNI KUPAMBANA NA WAONGO, WACHONGANISHI
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Fue Mlindoko akizungumza kwenye baraza la Wazazi |
Na Suzy Luhende , Shinyanga
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Fue Mlindoko amesema katika uongozi wake
Atatumia Sheria, Kanuni kupambana na waongo,wachonganisi wanaorudisha nyuma maendeleo ya Jumuiya.
Amesema hayo kwenye kikao cha Baraza la Jumuiya ya Wazazi kilichofanyika Septemba,28,2022 katika ukumbi wa CCM wilaya ya Shinyanga cha kuwachagua viongozi waliokuwa hawajachaguliwa, ambao ni katibu elimu malezi na mazingira na wajumbe wa kamati ya utekelezaji.
Mlindoko amesema hatopenda kusikia mambo ya uongo uongo katika Jumuiya, atawapenda watu wenye kutoa ushauri mzuri wa kujenga chama na kuleta maendeleo ndani ya chama na jumuiya hiyo.
"Nawaombeni sana viongozi wenzangu uchaguzi umeisha tufanye kazi kwa pamoja tushirikiane, ili jumuiya yetu iweze kusonga mbele, pia tutunze siri zetu za ndani za kimaendeleo na tufanye mabadiliko, ni vizuri tuweke alama nzuri katika Jumuiya yetu na kuitendea haki.
" Inatakiwa tuwe wazazi kweli tusimame katika eneo letu, kwa sababu sisi ndio wazazi walezi, tabia yangu ni kuleta mshikamano, tuwe na upendo wa hali ya juu tupendane zaidi na dhumuni letu ni kujenga timu yetu imara"amesema Mlindoko.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga Doris Kibabi amewaomba viongozi wote waliochaguliwa wawe viongozi wa mfano waonyeshe alama ya maendeleo wasiache madoa ambayo yatakuwa hayana faida kwa kizazi kijacho,pia wakemee masuala ya ukatili wanayofanyiwa watoto.
"Nina imani na viongozi mlionichagulia tutaanza kwa mchaka mchaka, pia viongozi wa kata nawaombeni muwe mnafanya vikao ndani ya miezi mitatu, kwani sisi wenyewe ndiyo tunaitengeneza Jumuiya yetu, mnatakiwa muonyeshe alama tusiache madoa ambayo yatakuwa hayana faida kwa kizazi chetu tufanye kitu chenye faida kwa kizazi chetu,pia tukemee matukio mbalimbali ya ukatili kwa watoto wetu na tusimamie masuala ya elimu ili watoto wetu watimize ndoto zao"alisema Kibabi.
Katika uchaguzi huo Richard Chacha Mseti alichaguliwa kuwa katibu elimu malezi na mazingira aliyeshinda kwa kura 51, wapiga kura walikuwa 56, pia walichaguliwa wajumbe wa kamati ya utekelezaji, ambao ni Zulfa Dali, Daniel Kapaya, Josephate Msozi, na Giti Mliga Boniface huku msimamizi wa uchaguzi huo akiwa ni Kudely Sokoine ambaye kabla alikuwa katibu elimu malezi na mazingira na kutogombea tena nafasi hiyo.
Picha:
Post a Comment