SIMBACHAWENE : UTAFITI UTAIWEZESHA SERIKALI KUFAHAMU TABIA HATARISHI
SERIKALI imezindua Utafiti wa Viashiria na Matokeo
ya Ukimwi Tanzania (THIS 2022-2023) na kueleza kuwa kiwango cha maambukizi mapya ya VVU na UKIMWI kimeshuka na kufikia asilimia 4.7.
Pia imedhamiria kudhibiti maambukizi ya VVU kwa kuongeza uelewa kwa wananchi, kujua hali zao za maambukizi ya VVU, kujiunga na huduma za matibabu ya VVU, kuongeza uelewa na ujuzi wa kukabiliana na janga hilo nchini.
Imeelezwa kuwa utafiti uliofanywa mwaka 2016/17 ulionyesha idadi ya wanaoishi na virusi vya Ukimwi waliojitambua ilikuwa 61%, waliokuwa kwenye tiba 92% na waliofikia ufubazaji VVU 87%, matokeo ambayo yalikuwa muhimu katika kuunda mkakati wa Kitaifa wa mwitikio wa VVU na UKIMWI.
Akizindua utafiti huo Septemba 29,2022 kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amesema utafiti utaiwezesha
serikali kufahamu tabia hatarishi zinazochangia kuenea kwa VVU na viashiria vinavyotoa taarifa hizo vitazingatia umri,jinsia, maeneo na nchi kwa ujumla.
“Sote tunafahamu kuwa takwimu bora ni muhimu katika kufahamu ukubwa wa janga la UKIMWI katika nchi yetu, tunaendelea kukusanya takwimu bora zitakazotupa uelewa wa hali ya maambukizi na namna ambavyo programu na afua za VVU zinavyofanya kazi ili kufikia malengo ya 95 ya Shirika la UKIMWI duniani na kudhibiti janga hili ifikapo 2030 " amesema.
Simbachawene amesema ili kufikia udhibiti wa janga hilo nchini,serikali inahitaji kuendelea kutathmini na kufuatilia kiwango cha maambukizi mapya, idadi ya watu wenye
maambukizo ya VVU, walio kwenye matibabu ya ARV za kufubaza VVU.
“Utafiti wa viashiria vya VVU na UKIMWI kwaka 2022/2023 utakuwa wa tano kufanyika nchini, utafiti uliopita wa mwaka 2016/2017 ulitoa mwanga juu ya namna tulivyoelekeza nguvu zetu kufikia malengo yaliyokusudiwa katika mapambano dhidi ya maambukizi
mapya ya VVU na UKIMWI,”
“Utafiti huo ulionyesha kiwango cha maambukizi nchini, kushuka na kufikia asilimia 4.7 na ulionyesha idadi ya wanaoishi na virusi vya Ukimwi waliojitambua 61%,
walio katika tiba 92% na waliofikia ufubazaji VVU 87%.” Ameeleza.
Waziri huyo wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu amesema tangu mwaka 2018, nchi imekuwa ikitekeleza kwa kasi afua zinazolenga kutambua wanaoishi naVirusi vya Ukimwi na kuwaunganisha kwenye tiba za ARV wafikie ufubazaji wa VVU,ili kufanikisha hilo, serikali ina jukumu la kuwahakiki wanaoishi na virusi vya Ukimwi kupitia tafiti kama hizi kwenye ngazi ya jamii na taifa kwa ujumla.
Amesema serikali kwa " utafiti huu kama ulivyokuwa wa mwaka 2016/2017 iatoa takwimu za VVU zitakazotupa uelewa zaidi wa kukabiliana na janga la UKIMWI, pia takwimu zitatuongoza katika kuboresha mipango ya
afya na mgawanyo wa rasilimali fedha katika program mbalimbali za VVU "amesema.
Simbachawene amesema si kila mtu anayeishi na VVU nchini Tanzania anafahamu hali yake,hivyo
utafiti wa THIS 2022-2023 utatoa fursa kwa kaya takriban 19,000 kupimwa VVU majumbani na kujua hali zao siku hiyo hiyo pia watafanyiwa kipimo cha ugonjwa wa homa ya ini ‘B’ na homa ya ini ‘C’ na hivyo kusaidia waliokutwa na maambukizi kupata huduma za afya.
“Watakaokutwa na maambukizi ya VVU kwenye utafiti huu wataunganishwa na vituo vya afya
watakavyochagua ili kuanza matibabu,huduma za ARV zinapatikana bure katika vituo vyetu vya afya, na matibabu yanasaidia watu wanaoishi na VVU kuishi
maisha marefu yenye afya na kupunguza hatari ya kuambukiza watu wengine,”amesema.
Mkurugenzi Mkazi wa ICAP,Haruka Mayaruma amesema utafiti huo ni sehemu ya mradi unaosimamiwa na ICAP unalenga kuongeza jitihada za kupambana na VVU zisingefanikiwa bila serikali,Kituo cha Dharura cha Magonjwa cha Marekani kwa kuwezesha tiba na matunzo kwa wanaoishi na VVU ili kupunguza vifo
na maambukizi mapya.
Amesema kaya 20,000 sawa na watu 40,000 wa umri kuanzia miaka 15 na kuendelea kote nchini zitafikiwa na utafiti huo utakaosaidia kufikia malengo ya 95-959-95.
Balozi wa Mareakani nchini,Dr. Donald Right amesema
jitihada zinazofanywa na serikali ya Tanzania zitasaidia mapambano dhidi ya UKIMWI ingawa eneo la mambukizi ya mtoto kutoka kwa mama halijaanya vizuri na kusistiza kujifunza kwa matokeo ya nyuma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kifua Kikuu na UKIMWI, Fatuma Towafiq amesema Bunge litaendelea kuishauri na kuisimamia serikali itenge bajeti ya VVU na anaamini utafiti huo ukifanyika kwa weledi na umakini utatoa matokeo sahihi yenye tija na kuwawezesha Watanzania kuwa an afya bora.
Naibu Katibu Mkuu Seif Shekilaghe, kwa niaba ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, amesema utafiti huo wa tano kufanyika utaonyesha namna ya kutekeleza mapambano ya VVU na utangalia magonjwa mengine ikiwemo homa ya Ini B na C ili kufikia malengo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dr.Leonard Maboko amesema za mwaka 2017 zilionyesha watu milioni 1.4 walikuwa na maambukizi mapya na mwaka 2021 watu milioni 1.7 walikadiriwa kuwa na maambukizi ya VVU.
“Asilimia 84 wanafahamu hali zao,73 asilimia wanafikiwa na huduma za afya na 66 asilimia wanatumia dawa za kufubaza virusi (ARV), hivyo
takiwmu za THIS 2022-2023 zitasaidia kutupima na kuwa na ujuzi wa masuala ya VVU,”amesema Maboko.
Henry Karugendo wa Taasisi ya Takwimu la Taifa (NBS)
Henry Karugendo amesema watashirikiana na Wiara ya Afya kupanga mipango mbalimbali ya afya kwa kutumia takwimu bora za VVU ambazo ni nyenzo muhimu ya kuiwezesha serikali na wadau kuandaa sera, mipango na takwimu rasmi za mapambano ya VVU kuhakikisha watu wanapata huduma za matibabu.
“Takwimu za utafiti wa THIS 2022-2023 zitaonyesha kiwango cha maambukizi mapya ya VVU, kiwango cha watumiaji dawa, kiwango cha homa ya ini B na C ni uelewa wa wananchi na kuisaidia serikali kuboresha huduma za afya,VVU na ustawi wa wananchi ".amesema.
Post a Comment