WANANCHI MISENYI WATAKIWA KUACHA TABIA YA KAKITANDUGAHO
Wahifadhi kutoka wakala wa huduma za misitu TFS wilaya ya Misenyi wakionyesha vifaa vya kuzimia moto kwenye misitu. |
Na Alodia Dominick, Misenyi
WANANCHI wilaya ya Misenyi mkoani Kagera wametakiwa kuacha tabia ya kuwaficha watu wanaowaona wakitenda makosa yakiwemo ya uhalifu kwa kuogopa kuwa wataonekana wabaya kwakuwa wametoa siri au taarifa maarufu kwa Kabila la Kihaya (Kakitandugaho).
Imeelezwa kuwa kitendo cha kutowataja wahalifu na kuendelea kufaya siri kimesababisha watu wazidi kuchoma moto ovyo misitu hali ambayo inaisababishia serikali hasara na wawekezaji wa misitu.
Mchungaji wa Kanisa la kiinjiri la Kirutheri Tanzania KKKT usharika wa Bugandika Mch. Christopher Mbuga alisema. " Watu wana tabia ya kakitandugaho wanamuona mtu anachoma misitu wanakaa kimya bila kumtaja mtu huyo aliyefanya uhalibifu wa kuchoma misitu hiyo kisa tu asionekane amesema anapotezea tu hiyo ni kakitandugaho.
Mchungaji wa kanisa la kiinjiri la Kilutheri Tanzania KKKT usharika wa Bugandika mch. Christopher Mbuga akizungumza na wenyeviti wa vijiji na vitongoji kata ya Bugandika. |
Baba Paroko wa Katoliki Parokia ya Bugandika Padre Deodatus Tiba alisema Binadamu wamejisahau wameanza kupinga uumbaji wa Mungu kwa kuchoma mimea ya asili hivyo akawataka wanamisenyi kumrudia Mwenyezi Mungu na kuacha vitendo vya uchomaji moto ovyo misitu lakini pia kuwataja wanaochoma misitu hiyo pindi wanapowaona.
Maarimu wa msikiti wa Bugandika Mudhihiri Uwesu aliwasisitiza wananchi kuwa na upendo kwa mali za wenzao na kuacha kutumiwa na shetani kwa kufurahia kuchoma moto ovyo misitu na kusababisha hasara.
Akitoa elimu kuhusiana na moto wa msituni Ofisa wa Zima moto katika ofisi ya Zima moto mkoa wa Kagera Thomas Majuto amewafundisha vyanzo mbalimbali vinazosababisha moto misituni kuwa ni pamoja na utayarishaji wa mashamba na kuchoma taka, kuchoma moto wakati wa uwindaji wa wanyama na ndege, urinaji asali kwa kutumia moto, uchomaji mkaa,upasuaji mbao, kuchoma moto kwa ajili ya kupata malisho mapya ya mifugo na moto unaotokana na radi.
Ofisa kutoka ofisi ya Zima moto mkoa wa Kagera Thomas Majuto akitoa elimu juu ya kuachana na tabia ya uchomaji wa misitu na athari zitokanazo na uchomaji moto |
Prukelia Frances ambaye amepata mafunzo hayo ameahidi kwenda kuwafundisha wenzake madhara yatokanayo na uchomaji moto misitu ambayo huathiri makazi ya wanyamapori na ndege, mazizi ya nyuki, husababisha kupotea kwa baadhi ya aina ya mimea au miti, huathiri kilimo na kuunguza mimea na viumbe hai visivyoonekana.
Muhifadhi wa Misitu (TFS) wilaya ya Missenyi Mrisho Juma amesema kuwa, wilaya hiyo inakumbwa na matukio mengi ya uchomaji moto misitu wakati wa kiangazi kuanzia Julai hadi Agosti kwani katika takwimu za mwaka jana inaonyesha matukio ya uchomaji moto yalikuwa 70 na Kwa mwaka huu wa 2022 matukio ya moto ni 60.
"Unaweza kuona ukubwa wa tatizo la uchomaji moto misitu lilivyo kwa wilaya ya Misenyi kwani Kwa mwaka 2021 matukio ya moto yaliyoripotiwa yalikuwa 70 na mwaka huu ni matukio 60" Alisema Juma.
Aliongeza kuwa wilaya ya Misenyi ina misitu 10 tisa inasimamiwa na TFS na msitu mmoja unasimamiwa na serikali pia kuna misitu mingine inayosimamiwa na vijiji na kwamba wataendelea kutoa elimu kwa jamii ili vitendo vya uchomaji moto misitu vipungue au kuisha kabisa.
Post a Comment