HEADER AD

HEADER AD

BODABODA WATAKIWA KUJIKINGA NA EBOLA

 Na Alodia Dominick,Bukoba. 

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amewataka waendesha pikipiki (Bodaboda) kuwa mabarozi wa kutoa elimu ya kujikinga na ugongwa wa Ebola wanapokuwa wakisafirisha abiria pamoja na kutoa tarifa kwa viongozi wa Kata, Kijiji,Mtaa na Kitongoji endapo watamuona mtu mwenye dalili za ugonjwa huo.


Waziri Ummy ameyasema hayo wakati akizindua  kampeni ya utoaji elimu kwa wakazi katika Manispaa ya Bukoba Octoba,6,2022 juu ya kujikinga na mlipuko wa ugonjwa huo hapa Nchini ijulikanayo "Tujikinge na Ebola iweke Tanzania  Salama".

"Bodaboda wanasafirisha watu kutoka eneo moja kwenda eneo lingine, nataka tuwatumie bodaboda kama watoa taarifa wakibeba abiria ambaye ana dalili za ebola watoe taarifa kwa kiongozi yeyote wa kata,kijiji na kitongoji.


      Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akitoa elimu ya ugonjwa wa Ebola

"Aseme amebeba abiria amemwacha sehemu fulani, amemuona ana kohoa, anahalisha au anatapika ili wafanye ufuatiliaji wa mtu huyo,bodaboda wachukue tahadhari kwa kunawa mikono na maji tiririka na sabuni" amesema Ummy.

Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Elimu kwa Umma Dk Ama Kasangala amesema serikali imetoa magari matano kwa ajili ya kampeini ya kuhamasisha juu ya kujikinga na ebola baada ya katibu mkuu wa wizara ya afya, Waziri wa afya na watumishi mbalimbali wa afya kupita maeneo mbalimbali mkoani Kagera hasa ya mpakani na kugundua kuwa kuna maeneo  yanapaswa kuongezewa nguvu.



"Tumetoa vizibao kwa bodaboda na frash zenye ujumbe wa ebola tunatarajia kugawa frash hizo kwa bodaboda 500 katika wilaya tano zenye hatari zaidi zitatolewa kwa bodaboda 100 kwa kila wilaya ambazo ni Kyerwa, Misenyi, Bukoba mjini, Karagwe na Muleba.


Mwendesha pikipiki Cletus Fabian amesema yupo tayari kutoa elimu popote atakapokuwa amebeba abiria na atakapoona mtu mwenye dalili za ebola atatoa taarifa haraka kwa viongozi.

Imeelezwa kuwa magari yenye mabango na ujumbe mbalimbali kutoka wizara ya afya kitengo cha utoaji elimu kwa umma yatakuwa yakipita maeneo mbalimbali kuelezea namna wananchi watakavyojikinga na ebola pamoja nakufahamu dalili zake.


Kwa mujibu wa Wizara ya Afya imeezwa kuwa,Ugonjwa wa Ebola ni ugonjwa wa hatari unaosababishwa na virusi vya Ebola.Ugonjwa ambao ni miongoni mwa magonjwa ya mlipuko yajulikanayo kama homa za Virusi zinazoweza kuambatana na kutokwa kwa damu mwilini.

Dalili za ugonjwa huo ni homa ya ghafla,maumivu ya misuli,kulegea kwa mwili,kuumwa kichwa,vidonda kooni,kutapika, kvipele vya ngozi,kutokwa damu sehemu za wazi za mwili kama vile macho,pua ,mdomo, na njia za haja ndogo na kubwa.

No comments