HEADER AD

HEADER AD

CAG YAOMBEA VIONGOZI KUTIMIZA MAANDIKO YA BIBLIA

 


 Dunstan Maboya,Askofu Mkuu wa kanisa la Calvary Assemblies of God,Ubungo Maziwa

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

KANISA la Calvary Tanzania Assemblies of God (CAG) 'Chuo cha Manabii',lililopo eneo la Bandari kavu,Ubungo Jijini Dar es Salaam linaendesha maombi maalumu ya wiki moja kuwaombea wakuu wa nchi na Tanzania kwa ujumla. 

Akizungumza wakati wa ibada Katibu wa Kanisa hilo Lucas John,amesema kuwa mombi hayo ni sehemu ya kutimiza maandiko katika Biblia kitabu cha 1Timotheo 2 : 1-2  kinachotaka maombi,sala na dua yafanyike kabla ya mambo yote ili kuishi katika utulivu na amani.

"Maandiko katika waraka wa kwanza kwa Timotheo 2:1-2 yanasema basi,kabla ya mambo yote,nataka dua,na sala na maombezi,na shukrani,zifanyike kwa ajili ya watu wote;kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka,tuishi maisha ya utulivu na amani,katika utauwa wote na ustahivu.

"Kufanya hivi ni katika kutii agizo hilo pamoja na kutekeleza moja ya majukumu ya msingi ya kanisa letu,tunawakaribisha watu kutoka sehemu mbalimbali jijini kuhudhuria maombi haya yatakayokuwa yakianzaa saa 11 jioni hapa kanisani "amesema Katibu.

Amesema maombi hayo yataongozwa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo,Imelda Maboya akishirikiana na viongozi wengine,yatakayoitimishwa jumapili Octoba 16,2022.

Ameongeza kuwa CAG ina makanisa zaidi ya 1500 Tanzania Bara na Zanzibar.


No comments