HEADER AD

HEADER AD

KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU AKAGUA KIWANDA CHA UCHAPAJI VITABU

 



Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Francis Michael amefanya ziara katika kiwanda cha uchapaji cha Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) cha Press A na katika maghala ya kuhifadhia vitabu yaliyopo katika eneo la  EPZA jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu amekagua kazi ya uchapaji wa  machapisho mbalimbali  inayoendelea kiwandani hapo pamoja na kazi ya usafirishaji wa vitabu vinavyosambazwa kwenda katika halmashauri mbalimbali nchini. 

Akihitimisha ziara yake, Katibu Mkuu ameipongeza TET kwa kazi nzuri inayofanya ya uchapaji na usafirishaji wa machapisho mbalimbali.


Ameiagiza TET kuandika maandiko yatakayoiwezesha  kupata fedha za kununua mashine za kisasa na zenye uwezo mkubwa  wa kufanya kazi ya uchapaji pamoja na kujenga ghala kubwa la kuhifadhia machapisho.

Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt.Aneth Komba amemshukuru Katibu Mkuu kwa kufanya ziara hiyo na kuifahamu TET kujionea kazi mbalimbali zinazofanyika na kuahidi kuyafanyia kazi maagizo aliyoyatoa.





No comments