HEADER AD

HEADER AD

WATOTO KUTONYONYA KWA WAKATI,SUMUKUVU CHANZO CHA UTAPIAMLO




Na Mwandishi Wetu,Itilima

MIONGONI mwa mambo yanayochangia hali ya utapiamlo ni pamoja na wazazi kutokuzingatia muda wa kunyonyesha watoto wao kufikia umri wa miezi 18 hadi 24 pamoja na uwepo wa kiasi kikubwa cha sumukuvu katika nafaka kutokana na uhifadhi duni.

Hayo yameelezwa na Afisa Lishe mkoa wa Simiyu Chacha Magige wakati wa mafunzo ya afya na lishe vijijini yaliyotolewa na shirika la pelum kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kupitia mradi wa agriconnect kipengele cha lishe.

Katika taarifa hiyo Chacha amesema wazazi na walezi hawazingatii ulishaji wa chakula cha nyongeza kwenye vyakula mchanganyiko na vyakutosha kwa watoto pamoja na kuelemewa na kazi nyingi za uzalishaji malu hivyo kukosa muda wa kutosha wa kula watoto wao.

"Ninawataka maafisa ugani kuhakikisha kwamba wananchi wanapata elimu ya namna ya kuzalisha mazao yenye virutubishi na namna nzuri ya kuyahifadhi ili yasishambuliwe na sumukuvu ambayo ni hatari Kwa afya watoto wetu" amesema Chacha.

Katika msimu wa kilimo 2021/2022 mkoa wa Simiyu ulizalisha choroko tani 2988, dengu tani 1698 mbaazi tani 885 maharage tani 985 na mazao ya kunde tani 826 kufanya uzalishaji wa mazao jamii ya kunde kuwa tani 7382.

Pamoja na kuwepo kwa chakula cha kutosha, mkoa unakabiliwa na tatizo la utapiamlo hususani udumavu kwa watoto chini ya umri wa miaka miatano ambao umeongezeka kutoka asilimia 26.1 mwaka 2014 hadi kufikia 31.2 2018.

Taarifa imeeleza changamoto nyingine za kilishe kwa watoto ni pamoja na ukondefu ulioongezeka kutoka asilimia 3 mwaka 2014 hadi 4.6 2018 na uzito uliokithiri kutoka asilimia 1.0 mwaka 2014 hadi 2.0 mwaka 2018.

Akielezea mkakati wa lishe wa Mkoa mkuu wa Mkoa huo Yahya Nawanda amesema mkoa unaelekeza kupunguza kiwango cha udumavu kutoka asilimia 31. 2 hadi kufikia chini ya asilimia 28 ifikapo mwaka 2025.

"Kwa kutekeleza utoaji wa elimu na unasihi wa lishe kwa wazazi juu ya ulishaji wa chakula mchanganyiko na cha kutosha kwa watoto wao sambamba na mkakati wa kutoa uji na chakula cha mchana kwa shule zote za msingi na sekondari mkoani hapa ifikapo 2025,".

Amewataka wataalamu kuwatambua na kuwapatia matibabu watoto wenye utapiamlo mkali na kutoa virutubishi vya nyongeza Kwa watoto na akinamama wajawazito Ili kupunguza uwezekano wa kupata utapiamlo. 

Akitoa nasaha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sofia Mjema kwa wazazi baada ya kuangalia namna ya kutengeneza uji ulioongezewa virutubishi katika mafunzo yalijojumuisha kinamama wenye watoto umri chini ya miaka miatano na watoto miaka 10 Hadi 15.

Mjema amewataka wazazi kuhakikisha wanakuwa kipaumbele katika kupiga vita hali ya utapiamlo kwa kutumia mafunzo waliyoyapata ili kuwanusuru watoto na magonjwa yatanayosababisha udumavu.

"Lishe liwe ni suala endelevu kwa jamii zetu, tunachakula cha kutosha tuache mazoea ya kula chakula cha aina moja kwa muda mrefu, tufuate wataalamu wa afya wanachokisema ili kuhakikisha kila mmoja anakuwa na afya njema, " amesema Mjema.

>>>Sumukuvu ni Kemikali
zinazozalishwa na aina ya fangasi/ukungu/kuvu wanaoota kwenye punje za nafaka,mbegu za mafuta,mikunde na mazao ya mizizi.

Sumukuvu pia hupatikana katika bidhaa za mifugo kama vile mayai nyama na maziwa iwapo watakula chakula kilichochafuliwa na sumu.


No comments