DKT. MPANGO AIAGIZA MAKUMBUSHO KUKUSANYA ALA ZA MUZIKI
Na Andrew Chale, Bagamoyo
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ameagiza Makumbusho ya Taifa kukusanya Ala za Muziki za mikoa yote hapa nchini ili ziweze kuhifadhiwa kulinda tamaduni za mtanzania.
Dkt. Mpango ametoa kauli hiyo Novemba 11, 2022 wakati akizindua Tamasha la 41 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni linalofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), Mkoani Pwani.
Makamu wa Rais ametembelea banda la makumbusho ya taifa la kushiriki tamasha hilo linaloonesha Ala mbali mbali za muziki za baadhi ya makabila ya hapa nchini pamoja na maonesho ya picha jongefu za kale katika masuala ya Sanaa na Utamaduni.
Makamu wa Rais Mhe Dkt. Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Elimu wa Makumbusho ya Taifa Anna Sonelo alipotembelea banda hilo la maonesho TASUBa. Picha na Andrew Chale.
Dkt. Mpango akiwa kwenye maonesho hayo ameelezwa namna makumbusho hiyo inavyofanya kazi zake kwa ukaribu na wasanii, kisha akatoa agizo hilo la kukusanywa ala za muziki kwa kila mkoa na kuzihifadhi kwakuwa baadhi upotea kutokana na ukuaji wa teknolojia.
Ametaka Ala hizo zikipatikana zihifadhiwe angalau ziweze kukaa miaka 200, ili vizazi vijavyo wazijue na kuona umuhimu wa Ala hizo za Muziki wa Tanzania. Baadhi ya Ala hizo za muziki ni Zeze, Ngoma, Marimba, manyanga na zinginezo.
Post a Comment