HEADER AD

HEADER AD

TAASISI ZATAKIWA KUFANYA TAFITI ZA KISAYANSI

Na Mwandishi wetu, Mwanza 

TAASISI mbalimbali hapa nchini zimetakiwa kufanya tafiti za kisayansi zitakazowezesha wananchi kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza na zijiwekeze katika kutoa huduma pamoja na kutoa mbinu mpya za matibabu.

Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.James Mdoe wakati akifungua kongamano la nne la kisayansi katika maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukiza mkoani Mwanza.

Prof. James amewataka wataalamu wa kisayansi kujadiliana juu ya matumizi ya dawa za asili ambazo zingine zimekuwa zikitumika kutibu pumu, shinikizo la juu la damu na Saratani.

"Tuweke mfumo sahihi wa kuwezesha dawa hizi za asili zikithibitika kisayansi kuwa zinatibu na hazina madhara basi tuweze kuzitumia kudhibiti magonjwa haya yasiyoambukiza.

" Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu inaendelea kufanya kazi na wadau wote wenye nia ya kusaidia mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza, kwani bila kufanya hivyo mlipuko wa magonjwa haya utaendelea kuua watu wengi, kuleta ulemavu na mwisho kurudisha nyuma jitihada za taifa kukuza uchumi," amesema. 


Prof. James amesema serikali inaendelea kuboresha miundombinu na kununua vifaa tiba vya kisasa vikiwemo vifaa vya uchunguzi vinavyowezesha wanasayansi kufanya kazi zao kiurahisi ili kugundua magonjwa mapema hususani yasiyoambukiza. 

Amesema huduma za uchunguzi na utambuzi wa magonjwa (Maabara), Mionzi na Radiolojia zimeboreshwa kwa maana ya miundombinu na vifaa vya kisasa ili kurahisisha utoaji huduma ya magonjwa yasiyoambukiza na uwezo wa kufanya tafiti mbambali za kisayansi.

Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Prof. Paschal Ruggajo amempongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kulipa kipaumbele swala la mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza na sasa ameipa kazi Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi, kifua kikuu kusimamia maswala ya Magonjwa Yasiyoambukiza. 

"Tunatambua mchango mkubwa wa Bunge katika  kuimarisha afya za watanzania." amesema Prof. Paschal.

"Hii kauli mbiu ya mwaka huu ni ya Badili Mtindo wa Maisha, Boresha Afya"  lengo lake kuu ni kuitaka jamii ya watanzania na wadau wote kushirikiana katika kubadili mtindo wa maisha ili kuwa na afya bora na yenye kuleta tija kwa Taifa letu." Amesema Prof. Paschal.


>>>Wizara ya Afya kupitia Idara ya Huduma za Tiba inaratibu kitengo na Mpango wa Taifa wa Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza, inatekeleza afua mbalimbali ili kuongeza nguvu ili kuweza kufikia malengo ya kuzuia na kudhibiti magonjwa hayo.




No comments