HEADER AD

HEADER AD

HALMASHAURI YATELEKEZA STENDI ILIYOFUNGULIWA NA DC


Na Dinna Maningo, Tarime 

HALMASHAURI ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara imetelekeza stendi ya Ng'ereng'ere iliyopo kata ya Regicheri kwa kushindwa kuiendeleza kujenga miundombinu rafiki ya stendi kwa kipindi cha miaka sita hali ambayo imesababisha mabasi, gari ndogo na malori kutoingia ndani ya stendi.

Stendi ya Ng'ereng'ere ilifunguliwa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga tarehe 1, Agasti, 2016 ambapo vilijengwa vyumba viwili vya mfano ambavyo ni kituo cha polisi na ofisi ya mkuu wa stendi.

DIMA Online Novemba, 10, 2022 imefika katika stendi hiyo na kukaa kwa zaidi ya masaa matano ili kujionea hali halisi kama mabasi yanaingia ndani ya stendi hiyo. 

Mwandishi wa chombo hicho cha Habari hadi anaondoka katika eneo la stendi majira ya saa 11 jioni, basi moja pekee la Zakaria T 784 DHY ndio lilionekana kuingia stendi huku mabasi mengine yakionekana kuunga safari moja kwa moja kwenda Sirari na mjini Tarime bila kuingia ndani ya stendi hiyo.


Bas la Zakaria likiwa stendi

DIMA Online imeshuhudia kuona eneo la stendi hiyo likiwa limezungukwa na nyasi , huku mbuzi, ng'ombe na kondoo wakila nyasi, pembeni kukiwa na waendesha bodaboda wakiwa kwenye eneo lao la maegesho pembeni ya stendi hiyo.

Katika eneo hilo la stendi kumeweka vibao mbalimbali vyenye maandishi  yanayosomeka  maegesho ya malori, maegesho gari ndogo, maegesho gari za abiria Musoma/ Mugumu, kuingia Malori, kuingia Mabasi  na kutoka.

Eneo hilo upande wa mashariki kuna jengo lenye vyumba viwili vilivyokamilika ujenzi vilivyopakwa rangi ambapo chumba kimoja kikiwa kimeandikwa maandishi juu ya mlango yanayosomeka ofisi ya mkuu wa stendi ikiwa kimefungwa kwa kufuli na chumba kilichoandikwa kwa maandishi yasomekayo kituo cha polisi kikiwa wazi nje ya kituo hicho akionekana kijana wa kiume aliyevaa mavazi ya kiraia.

      Kituo cha polisi na ofisi ya mkuu wa stendi

Vyumba vingine vinne vimeonekana ujenzi wake haujakamilika umefikia hatua ya boma, pembeni kukiwa na kontena linalotumika kama ofisi ya serikali ya kijiji cha Ng'ereng'ere pamoja na jengo lenye chumba kimoja lililojengwa na mwananchi kama kibanda ambalo ujenzi wake umefikia hatua ya boma.

Katika eno hilo la stendi kuna choo chenye matundu matano, na upande mwingie wa eneo kumejengwa jengo dogo la abiria mbele kukiwa na kichuguu cha mchwa.


                            Choo

Kwakuwa stendi hiyo halitoi huduma kama ilivyokusudiwa vijana wa kijiji cha Ng'ereng'ere wameamua kuliendeleza eneo hilo kwa kulitumia kucheza mpira wa miguu ili kufanya mazoezi ya viungo kuhimalisha afya ya mwili.

        
            Jengo la abiria


    Stendi yatumika kwa michezo





Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Luoga akifungua stendi akiwa na aliyekuwa mkurugenzi wa Halmshauri ya wilaya ya Tarime Apoo Tindwa na viongozi wengine wakishuhudia ufunguzi. Agasti, 1,2016.



      Hali ilivyokuwa siku ya ufunguzi wa stendi 



No comments