HEADER AD

HEADER AD

KANALI NGEMELA AWATAHADHALISHA WAPIGA KURA CCM MARA



Na Jovina Massano, Musoma

MSIMAMIZI Mkuu wa Uchaguzi wa Viongozi Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Mara, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga amewaeleza wapiga kura kuwa hitaji la Chama ni kuona wapiga kura wakichagua viongozi wanaoleta maendeleo ndani ya chama na kwa wananchi.

Ameyasema hayo kabla ya wagombea kuanza kuomba kura kwa wajumbe katika uchaguzi unaoendelea ndani ya viwanja vya ofisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa.

Msimamizi huyo kutoka Makao Makuu ya Chama hicho Jijini Dodoma amewaeleza wajumbe kutambua kuwa CCM inahitaji viongozi wanaoendana na hitaji la wananchi.

           Msimamizi wa Uchaguzi

 "Mkoa unaweza ukawa hauna maendeleo lakini wakapatikana viongozi stahiki wenye kuleta maendeleo hivyo msichague viongozi mpechempeche kwa maana ya legelege ili kuleta maendeleo shahiki", amesema Kanali Lubinga.

Amezitaja baadhi ya sifa za kiongozi kuwa, ni yule mwenye uwezo wa kukutana na mazingira tata akayatatua na atakayeweza kujenga Chama imara  na huo ndio mwanzo wa kupata Chama imara kitaifa.

Masha Matiku Mjumbe wa wa Mkutano Mkuu Wilaya ya Rorya amempongeza msimamizi huyo kwa kutoa elimu kwa wajumbe na kuwapa mwanga wa kuweza kufanya maamuzi sahihi kwa maslahi ya chama na kwa wananchi.
 
Ameongeza kuwa usia huo utasaidia kuondoa makundi na kutoleta mpasuko ndani ya Chama hivyo wajumbe wanapaswa kuufanyia kazi.

                      Wajumbe

No comments