HEADER AD

HEADER AD

MAENEO YA UWANJA WA NDEGE, MIPAKA KUDHIBITIWA KUJIKINGA NA EBOLA

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

SERIKALI inaandaa Mpango madhubuti katika maeneo ya uwanja wa ndege pamoja na maeneo ya mipaka ili kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ebola nchini, ambapo imeweka wataalamu kwaajili ya kuhakikisha wanaoingia nchini wanafuatiliwa kwa uangalizi.

Akizungumza Novemba 14,2022 Jijini Dar es Salaam Mratibu wa Ufuatiliaji na Udhibiti  wa Magonjwa, Dkt.Vida Makundi amesema hayo wakati akifungua mafunzo kwa wahudumu ngazi ya jamii ambao kazi yao itakuwa kuwafuatilia wale ambao watakuwa wamekutana na wagonjwa wa Ebola na kutoa taarifa.

Amesema katika harakati za kujiandaa kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa Ebola, wanajiandaa na zoezi la kufuatilia watu waliochangamana na mgonjwa wa Ebola endapo kwa bahati mbaya atakuwa amepatikana.

"Ufuatiliaji wa wasafiri ambao wametoka Uganda na sehemu nyingine ambao wanaweza wakawa wamekutana na wagonjwa tunawafuatilia kwa kuwahoji kila siku kama wanadalili zozote ambazo zinafanana na kuwa na dalili za Ebola". amesema 

Amesema inaaminika mgonjwa wa Ebola kama amekutana na mtu kati ya siku mbili mpaka siku 21 kama mtu amepatwa na maambukizi ndipo atakapoona dalili, hivyo wanafundisha makundi mbalimbali ya wafuatiliaji.


Amesema wahudumu ngazi ya jamii watakuwa wanatumika endapo ikahitajika kuwafuatilia wale ambao wamekuwa wamekutana na wagonjwa na watakuwa wanatoa taarifa kwa viongozi wao ambao ni maafisa afya ndani ya kata ambao watakuwa wanatoa taarifa kwenye halmashauri zao.

Ameongeza kuwa wahudumu ngazi ya jamii pia watakuwa wakifuatilia tetesi za magonjwa ndani ya jamii, wakipata tetesi ya mgonjwa yeyote ambaye yanaonekana yanaambukiza, yanahatari ya kuambukiza watoe taarifa kituo chochote cha afya kilichopo karibu au kwa afisa afya ngazi ya kata na taarifa zinakwenda juu kwaajili ya uchunguzi.




No comments