HEADER AD

HEADER AD

NMB YATEKELEZA OMBI LA DC KALAMBO,YATOA MABATI 600


Na Mwandishi Wetu, Kalambo

BENK ya NMB imetoa msaada wa mabati 600 katika Zahanati ya Kijiji cha Kapozwa wilayani Kalambo iliyoezuliwa paa na upeo.

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Tano Mwera ameishukuru benki hiyo kwa msaada wa mabati wakati alipotembelea  na kukagua ukarabati wa Zahanati ya Kijiji cha Kapozwa unaoendelea.

Amesema kuwa, akiwa katika ziara yake siku za nyuma alitembelea Kijiji hicho na kupewa kero hiyo ya Zahanati kuezuliwa paa na upepo mkali.

         
        Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Tano Mwera akiwa katika mkutano wakati alipotembelea ukarabati wa Zahanati ya Kapozwa, ambayo imechangia mabati 600 benki ya NMB.

"Nilifika hapa nikachukua kero hii, na kuomba msaada kwa Benki ya NMB, wakapokea kilio hicho na kutoa msaada wa mabati 600, bati hizo pia zitatumika kukarabati Zahanati za Vijiji vya Mambwekenye na Mpanga." amesema DC Tano.

DC huyo ameongeza kuwa serikali inatambua changamoto mbalimbali hivyo wataendelea kuzitatua kwa nguvu zote kwa kushirikiana na wadau wa sekta binafsi ikiwemo Benki hiyo ya NMB na wadau wengine katika kusaidia utendaji bora wa Rais Samia Suluhu.


        Muonekano wa jengo la Zahanati ya Kapozwa lililoezuliwa paa zake na upepo mkali hivi karibuni.


No comments