HEADER AD

HEADER AD

PROF.NAGU: WAGANGA WATOE DAWA KULINGANA NA MAJIBU YA MAABARA



Na Andrew Chale, Dar es Salaam.

MGANGA Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu amewaagiza Waganga na Madaktari nchini kutoa dawa kwa wagonjwa kulingana na majibu ya kimaabara ili kutambua dawa gani sahihi ya kutibu ugonjwa husika kuepuka usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa.

Ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam katika wiki ya kampeni ya kuzuia usugu wa vimelea dhidi ya dawa za Antibiotiki inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 18-24 Novemba ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘’Kwa pamoja tuzuie usugu wa vimelea dhidi ya dawa’’amesema.

Prof. Nagu amesema usugu wa dawa husababishwa na mambo mengi ikiwemo kutofuata usahihi wa matumizi na pia kukwepa kutumia wataalam wa hospitali.

‘’kwa sasa usugu wa vimelea vya dawa umeongezeka moja wapo ni kutotumia dawa kwa usahihi, mfano mtu unaambiwa utumie dawa kwa siku tano, wewe unatumia kwa siku mbili unapopata nafuu unaaacha hapa unajenga usugu kwa sababu havijaisha mwilini mwako.

Mganga Mkuu wa Serikali (CMO),Prof. Tumaini Nagu akizungumza katika kongamano la wiki ya Kampeni ya Kuzuia Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa, Jijini Dar es Salaam.

"Lakini pia kutumia madawa kabla ya hujapimwa, waapo wanaoenda duka la dawa hawajaonwa hata na Daktari, wao wanaenda kuchukua dawa bila kupimwa pindi wanapojisikia vibaya wanapewa hizi dawa za Antibiotiki, waananchi wote, unapojisikia vibaya tumia huduma zetu za afya.

Ameongeza kusema " Nenda hospitali yoyote iliyopo jirani, umuone daktari akupime, na ukiwa umeonekana na vimelea atachukua 'sampuli' atapeleka maabara vitapimwa.

" Kwa hiyo katika hili niwaombe pia Waganga madaktari, watumie hizi huduma za maabara kuangalia kama mtu anaugonjwa ilikujua anatumia dawa gani katika kukabiliana na ugonjwa husika.’’ Amesema Prof. Nagu.

Prof. Nagu amesema kwa sasa usugu kwa Tanzania unakadiriwa kuwa kati ya Asilimia 59.8 hadi 60, amesema vimelea vipo aina nyingi na dawa zipo za aina tofauti, hivyo ametoa rai dawa za Antibiotiki ziachwe kutumika kiholela na zaidi zitumike kulingana na ushauri wa kitaalam.


‘’Vimelea vikiwemo mwilini lazima tutumie Antibiotiki, lakini tutumie kwa uangalifu kulingana na wataalam, lakini pia tuweke mazingira ya usafi ya kujilinda ikiwemo kuosha mikono mara kwa mara, kusafisha Vyoo na usafi wa mwili  ilikuepuka magonjwa.

"Hivyo niwaombe watu wote wananchi, tujaribu kujikinga kwa kuboresha usafi wa mazingira, kuosha vyoo na vitu vingine vingi katika hali ya usafi.’’ amesema Prof. Nagu.

Amesema usugu wa dawa unatofautiana kulinagana na utumiaji wa madawa, katika hospitali moja na nyingine kulingana na mpangilio kazi wao wa utoaji wa madawa kwa wagonjwa wao na matumizi ya hospitali husika.

Katika kongamano hilo ambalo linatarajiwa kufikia tamati leo, wadau mbalimbali wameweza kuwasilisha mada za kibobezi katika sekta ya afya ikiwemo ya madawa ya binadamu na mifugo dhidi ya kukabiliana na usugu wa vimelea dhidi ya dawa.






No comments