CCM YASHIRIKI MKUTANO WA CHAMA TAWALA ANC NCHINI AFRIKA KUSINI
Na Cosmas Makongo, Johanneburg
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu ametuma ujumbe ukiwakilishwa na viongozi watatu wa CCM katika Mkutano wa 55 wa Chama cha Tawala AFRICAN NATIONAL CONGRESS nchini Africa kusini ambacho kimefanya uchaguzi mkuu wa kumchagua Mwenyekiti wa Chama hicho atakaye Gombea nafasi ya Urais Mwaka 2024.
Matokeo ya uchaguzi wa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha ANC yametangazwa Desemba, 19, 2022 mjini Johannesburg ambapo Rais Cyril Ramaphosa ameibuka mshindi kwa kuchaguliwa tena kwa mara ya pili kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho kwa kupata kura 2476 baada ya kumshinda mpinzane wake aliyepata kura 1897 Cde Zweli Mkhize ambapo jumla ya kura zilizopigwa ni 4393.
Katibu wa siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Mapinduzi Col.Ngemela Lubinga akiongoza ujumbe wa viongozi wa Chama cha Mapindizi amemkabidhi zawadi iliyotolewa na Mwenyekiti wa CCM Dkt Samia Suluhu akimpongeza kwa ushindi Mwenyekiti wa ANC Cyril Ramaphosa.
Ujumbe wa Tanzania ukiwakilisha Chama cha Mapinduzi katika mkutano wa ANC, uliwakilishwa na watu 3 ukioongozwa na Col.(mst). Ngemela Lubinga. Cde Ramaphosa ambaye ni kipindi chake cha pili na cha mwisho kuongoza chama hicho.
Post a Comment