HALMASHAURI YA MAFIA YAPEWA MSAADA WA DAWA
Na Mwandishi Wetu, Mafia
MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba nchini (TMDA) Kanda ya Mashariki imekabidhi msaada wa dawa za binadamu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Mkoa wa Pwani zenye thamani ya zaidi ya Milioni 6 kwa lengo la kusaidia matibabu ya wananchi wenye uwezo mdogo.
Dawa hizo zimekabidhiwa na Mkaguzi wa Dawa Japhari Saidi kwa niaba ya Meneja wa TMDA Kanda ya Mashariki (Bw Adonis Bitegeko).
Akikabidhi dawa hizo mbele ya Kamati ya Dawa na Vifaa Tiba (CFDC) ya Halmashauri ya Mafia Japhari ameeleza kuwa lengo la kukabidhi msaada huo wa dawa ni kusaidia wananchi wenye uwezo mdogo au wasio na uwezo kabisa kuchangia gharama za matibabu ili nao wapate dawa zenye ubora, usalama na ufanisi uliothibitishwa na TMDA.
"Dawa hizi zinatokana na sampuli zilizobaki baada ya uchunguzi wa kimaabara kukamilika na kufaulu vipimo.Hivyo, Ndugu Mkurugenzi naomba uzipokee ili ziweze kutumika kusaidia matibabu ya wananchi wa Mafia" Alisema Bw Japhari Saidi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mafia, Mwl Kassim Ndumbo ameishukuru TMDA, kwa msaada huo na kuomba iendelee kutoa msaada kwa maslai ya Wananchi wa Wilaya ya Mafia.
Post a Comment