HEAGTON YAPASUA, 37 KATI YA 52 WACHAGULIWA SHULE MAALUM
Na Dinna Maningo, Tarime
BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA) limewachagua wanafunzi 37 waliohitimu darasa la saba na kufaulu mitihani Katika shule Binafsi ya Msingi Heagton iliyopo katika Kijiji cha Ng'ereng'ere Kata ya Regicheri katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara, kwenda kujiunga kidato cha kwanza shule maalum kwa mwaka 2023 huku 15 wakipangiwa shule za kutwa.
DIMA ONLINE imetembelea tovuti ya NECTA kuona shule za Wilayani Tarime ambazo zimefanikiwa wanafunzi kuchanguliwa shule maalumu nakubaini shule hiyo ya Heagton kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi 37 Kati ya 52 waliochaguliwa.
Jumla ya wanafunzi 21 wamechaguliwa kwenda kujiunga kidato cha kwanza Bweni Kitaifa, wanafunzi 7 kwenda shule za vipaji maalum na wanafunzi 9 wamechaguliwa kwenda shule za ufundi kwa mwaka 2023
Heagton imeishika nafasi ya kwanza katika mkoa wa Mara wenye jumla ya shule za msingi 855 zilizopo kwenye orodha ya wanafunzi waliochanguliwa kujiunga na elimu ya Sekondari.
Heagton imeshika nafasi ya kwanza katika shule 170 Wilayani Tarime, shule hiyo ikiwa na jumla ya wanafunzi 52 waliopangiwa shule maalum na shule ya kutwa.
Awali katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2022 shule ya msingi Heagton katika mtihani wa kuhitimu darasa la saba ilisajili wanafunzi 52, wote walipata wastani wa A na hivyo kushika daraja la A.
Ada inayolipwa katika shule hiyo ni kati ya Milioni 1 hadi Milioni 1.8 kutegemea na madarasa na huduma anayotumia mwanafunzi.
Mkuu wa Shule ya Msingi Heagton Mwl.Thobias Samas ametoa wito kwa wazazi na walezi kwamba, kama wanatamani watoto wao wapate elimu bora basi Heagton ni shule sahihi itakayotimiza azima hiyo.
Wafanyakazi wa Heagton
" Tuna walimu wenye weledi na uzoefu wa kutosha katika kufundisha na wanayamudu vizuri masomo wanayofundisha...hivyo nawakaribisha sana wazazi na walezi kuleta watoto wao Heagton pre and primary school" amesema Mwl. Thobias.
Katika Halmashauri ya Mji Tarime ni shule mbili pekee za Binafsi kati ya shule 35 zilizopo katika Halmashauri hiyo zimefanikiwa wanafunzi kupelekwa shule maalum ambazo ni St. Jude wanafunzi watatu wamechaguliwa kwenda shule za vipaji maalum na wanafunzi wanne kwenda shule za ufundi ikiwa na jumla ya wanafunzi 86 waliopangiwa shule maalum na kutwa.
Shule Binafsi ya Muderspach Memorial Adventist wanafunzi wawili wamechaguliwa kwenda shule za vipaji na wanafunzi wawili kwenda shule za ufundi ikiwa na jumla ya wanafunzi 70 waliopangiwa shule maalum na kutwa.
Licha ya shule Binafsi kuwa na ada kubwa kati ya 800,000- hadi Milioni 1.9 b shule binafsi zilizosalia hazijabahatika wanafunzi kuchanguliwa kwenda kujiunga kidato cha kwanza shule maalum hivyo wote wamechaguliwa shule za kutwa.
Shule za Serikali Wilayani Tarime hakuna iliyopenya wanafunzi kuchaguliwa kwenda shule maalumu huku baadhi ya shule Binafsi maarufu nazo zikiangukia pua kwa kutochaguliwa wanafunzi kwenda shule maalumu licha ya kuwa na ada kubwa.
Baadhi ya shule hizo za Binafsi maarufu ambazo hazijapenya ni shule ya msingi Pope John II, St. Magreth, St. Catherine Labour'e, St. Michael, Maryo, Mary Immaculate na St. Agustino katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.
Shule zingine maarufu za Binafsi zilizopo Halmashauri ya Mji Tarime ambazo hazijapenya wanafunzi kuchaguliwa kwenda shule maalum ni Msati Hill Crest, Heaven na Mwera Vision.
Post a Comment