JOYCE MANG'O AFUNGUA MAFUNZO YA UONGOZI, ASISITIZA USHIRIKIANO UWT
Na Jovina Massano, Bunda
MJUMBE wa Halmashuri Kuu ya Taifa (NEC ) kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Bara, wa Chama cha Mapinduzi ( CCM), Joyce Mang'o amefungua mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa umoja huo Wilayani Bunda Mkoani Mara.
Mafunzo hayo yametolewa kwa viongozi 176 kutoka Kata 14 na matawi 69 yaliyofanyika ukumbi wa Harriet Wilayani humo ambayo yamewahusisha Makatibu na Wenyeviti wa UWT kuanzia ngazi ya Wilaya, Kata na Matawi.
Mafunzo hayo ni moja ya agizo la Mwenyekiti Taifa Dkt. Samia Suluhu alilolitoa katika hotuba yake makao makuu ya Chama jijini Dodoma mara baada ya uchaguzi ngazi ya Taifa kukamilika.
Akifungua mafunzo hayo Joyce amewaasa viongozi hao wa UWT kutokuwa na makundi na badala yake wajielekeze katika uletaji wa maendeleo katika chama na kwa jamii ya mkoa wa Mara.
MNEC kupitia UWT, Joyce Mang'o akizungumza na wanawake wa UWT Bunda wakati akifungua mafunzo ya uongozi
"Kwanza naomba niwashukuru Mwenyekiti na Katibu wa UWT kwa kutelekeza agizo alilolitoa Mwenyekiti wetu wa Taifa Dkt. Samia Suluhu kuhakikisha kila kiongozi anapata uelewa mpana wa uongozi na wajibu wake kwa nafasi aliyonayo", amesema Joyce.
Amewakumbusha kuwa, uchaguzi umeshapita hivyo ni wakati wa kuchapa kazi ya kuongeza idadi ya wanachama, amesisita umoja, mshikamano na amani kwa wanawake wote.
" Ukitaka kufanya mambo haraka fanya peke yako ila ukitaka kwenda mbali nenda na wenzio maendeleo ya UWT yatawenzekana kwa ushirikiano, ongezeko la wanachama wapya ni juhudi za viongozi katika uwajibikaji kwa kusimamia sera na mwongozo wa katiba ya chama ili kuzidisha uhai wa umoja huo.
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Bunda Marysiana Sabuni amesema Rais Samia anafanya kazi kwa vitendo sio maneno hivyo utekelezaji huo wa uelimishaji viongozi ni wa msingi kwa kuwa wengi wao walikuwa wanachaguliwa kuwa viongozi hawajui wajibu wao katika uongozi.
"Tunamshukuru sana mjumbe wetu wa Halmashauri Kuu UWT Bara Joyce kwa ushirikiano wake wa kutuunga mkono kukubali kuja kutufungulia mafunzo yetu hii inaonyesha ukomavu na utii kwa Chama tulipomshirikisha alikubali ombi letu", amesema Sabuni.
Katibu wa UWT katika Wilaya hiyo, Evodia Edward amesema utaratibu huo wa elimu kwa viongozi ulikuwepo tangu zamani tatizo ilikuwa ni utekelezaji wake kwa viongozi kutolisimamia na ilikuwa changamoto kulitekeleza.
Ameongeza kuwa, elimu hiyo ya wajibu na majukumu ya viongozi itasaidia kuamsha uwajibikaji na kila mtu kutambua nafasi yake ya uongozi kuanzia chini kwenye matawi kwani huko ndipo kulipo na chimbuko la upatikanaji wa wanachama na viongozi, amewahimiza watakaopata mafunzo hayo wahakikishe wanatoa elimu hiyo katika maeneo yao.
Post a Comment