HEADER AD

HEADER AD

RAAWU YAWATAKA WATUMISHI KUANZISHA MIRADI KABLA YA KUSTAAFU

 
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

CHAMA cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Ufundi Stadi, Habari na Ushauri (RAAWU) kimewashauri watumishi kuanzisha miradi mapema kabla ya kustaafu.

Ushauri huo umetolewa na Katibu Mkuu wa RAAWU, Joseph Shayo wakati wa mkutano wa mwaka wa watumishi wa Makumbusho ya Taifa uliofanyika jijini humo ambapo amesema kuwa, kuna umuhimu wa kuanza miradi ya kuongeza kipato wakiwa bado kazini.


"Unajiona kijana kwa sasa lakini itafika muda wa kustaafu hivyo ni muhimu kuanza kujiandaa kustaafu" amesema  Shayo.

Amesema wastaafu wengi huanzisha miradi baada ya kustaafu jambo ambalo linakuwa halina mafanikio na hivyo kutofanikiwa vizuri.

Amewataka watumishi hao kufanyakazi kwa bidii na maarifa kwa manufaa ya Taasisi na taifa kwa ujumla lakini pia wajiunga na chama cha wafanyakazi ili waweze kuunganisha nguvu za kutetea haki za  wafanyakazi.




No comments