KAMISHNA MWAKILEMA ASISITIZA USHIRIKIANO NA WATENDAJI
Na Mwandishi Wetu, Arusha
KAMISHNA wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), William Mwakilema amewataka viongozi wa shirika kushirikiana na watendaji wengine katika kupanga mikakati ya pamoja ya kazi ili kuleta ufanisi.
Kamishna Mwakilema ameyasema hayo Desemba, 13, 2022 wakati akimuapisha Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, James Paschal Kidubo msimamizi wa ukaguzi wa ndani katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya TANAPA jijini Arusha.
“Washirikisheni watendaji mnaofanya nao kazi ili kuwa na mikakati ya pamoja. siku zote maamuzi yanayozingatia maoni ya watalaamu huwa yana tija” alisema
“Utafanya maamuzi kama kiongozi lakini kwa kushirikisha watendaji wengine itafanya kazi yako iwe nyepesi” alisisitiza Kamishna Mwakilema.
Kamishna James Paschal Kidubo ameahidi kufanya kazi kwa bidii na kushirikiana na watendaji wengine. “Natambua majukumu haya ni makubwa na ninaahidi kupokea na kufanyia kazi maoni na ushauri kutoka kwa wasaidizi wangu na pia maelekezo kutoka kwa viongozi.” alisema.
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Richard Kafwita amesema Kamishna Kidubo ana elimu ya shahada ya Uzamili katika masuala ya fedha (Master of Science in Finance) kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde nchini Uingereza kwa ushirikiano na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es salaam, na ana cheti cha uhasibu (CPA). Kamishna Kidubo aliajiriwa TANAPA tangu mwaka 2013.
Post a Comment