HEADER AD

HEADER AD

WATOTO ZAIDI YA 50 KUSHIRIKI SHUJAA COMMANDO CAMP 2022


Na Andrew Charle, Dar es Salaam

SHUJAA Kids inayoendesha mazoezi ya kishupavu kwa vijana wadogo wa kike na kiume nchini, inatarajia kufanya mashindano na mafunzo ya kishupavu yatakayowahusisha vijana zaidi ya 50, ambao watakuwa porini katika Msitu wa Pande (Pande Game  Reserve) na kupita kweneye vizingiti, na viunzi, Desemba 21,2022.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Shujaa Kids, Daniel Kijo amesema , mashindano yatawakutanisha wanafunzi hao vijana hao walio na umri wa miaka kati ya 4 hadi 13 wakiwa sambamba na Wazazi wao.

Daniel amesema kutakuwa na wakufunzi na washauri mahususi wa masuala ya kujiokoa na kujilinda yatakayofanyika kwa siku mbili Desemba 19-20.

Amesema watafanya mashindano hayo eneo la Oasis Village & Club, Mbezi Beach na baadae kilele cha fainali watafanyia Mabwepande katika  msitu wa Pande (Pande Game Reserve)ambao unamilikiwa na Wizara ya  Maliasili na Utalii.

"Hadi sasa tunamtegemea wanafunzi vijana hao wadogo zaidi ya 50 watakaoshiriki, watafanya mashindano na mafunzo, lengo ni kujenga ushujaa, lengo letu kuunganisha watoto na wazazi na kufanya familia za kitanzania kujiamini zaidi, na kuwa  vizuri zaidi.

"Kwa hiyo hata wazazi siku hiyo ya Desemba 21 watashirikiana  pamoja na watoto wao ikiwemo kupita kwenye viunzi, kuning'inia kwenye kamba, kupita kwenye matope, na maeneo mengine mengi ya michezo hiyo ya kikomando", alisema Daniel Kijo.

Amesema kuwa, hadi sasa Shujaa Kids imetimiza mwaka mmoja tokea ilipoanza rasmi November 21,2021, ambapo tayari wameshafanya mashindano makubwa manne ambayo wanayafanya kila baada ya miezi mitatu pamoja na mafunzo ya kila mwishoni mwa wiki hadi sasa wameshafanya 8 na kufanya kuwa na mafunzo 12 ndani ya mwaka mmoja hadi sasa

"Jamii imepokea mafunzo haya kwa upendo sana, wazazi wanaona watoto wanahitaji ushupavu, wanakaa nyumbani wanachezea simu wanacheza magemu kwa hiyo Wazazi wametupokea vizuri sana.

Katika shindano hilo la Shujaa Commando Camp 2022, washiriki wanatarajiwa kupatiwa vyeti vya ushiriki, Medali na zawadi mbalimbali.


No comments