HEADER AD

HEADER AD

MBUNGE NJALU AAHIDI USHIRIKIANO NA SMPC


Na Mwandishi Wetu Simiyu

MBUNGE wa Jimbo la Itilima Mkoani Simiyu, Njalu Silanga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) amesema yupo tayari kutoa ushirikiano na kuwatetea Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Sumiyu katika kuhakikisha wanafanya kazi zao katika mazingira mazuri.

Mbunge Njalu ameyasema hayo Desemba, 30, 2022, kwenye mkutano maalumu wa Chama cha Waandishi wa Habari katika Mkoa huo, uliofanyika  mjini Bariadi wakati akikabidhiwa cheti cha heshima na Chama hicho kutokana na mchango wake uliotukuk kwenye Taasisi hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2012 mpaka sasa.

Njalu ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo amesema " Nawashukuru viongozi, na wanachama wa SMPC kwa kutambua mchango wangu, ninawaahidi kuendelea kuwa mtetezi wa waandishi wa habari Mkoa wa Simiyu kila wakati" amesema.

Mbunge huyo amehaidi kuendelea kutatua changamoto mbalimbali zilizopo kwenye chama ikiwemo miradi ya kuendesha klabu huku akihaidi kuwa mlezi wa klabu hiyo.

Kabla ya kukabidhiwa cheti hicho cha heshima, Mwenyekiti wa Klabu hiyo Frank Kasamwa, amemtaja Mbunge huyo kama mdau mkubwa kwenye klabu hiyo ndani ya Mkoa, kwakuwa amekuwa msaada mkubwa katika kuhakikisha klabu na waandishi wa Habari wanafanya kazi katika mazingira mazuri.


Amesema kuwa klabu pamoja na wanachama wake kuna nyakati wamekuwa wakipitia kipindi kigumi, lakini mbunge huyo amekuwa pamoja nao wakati wote, huku akiwa mstari wa mbele katika kusaidia kutatua baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili.

" Kama klabu tunakushukuru sana Mbunge, ndiyo maana leo tumeona tukutunuku cheti hiki cha heshima kwa kutambua mchango wako mkubwa kwetu, umekuwa kiongozi na mwasiasa wa kuingwa.

" Umekuwa kiongozi mwenye msaada mkubwa kwa Klabu yetu, lakini pia kuwa msaada mkubwa kwa wanachama ambao wamekuwa wakipata matatizo mbalimbali," amesema Kasamwa.



No comments