HEADER AD

HEADER AD

RAIS MWINYI ASEMA SERIKALI INAFUATILIA VITENDO VYA UHALIFU


Na. Andrew Chale, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Hussein Ali Mwinyi amewaomba wananchi kuwa na uvumilivu kwakuwa Serikali inafuatilia mambo yote yanayotendeka yakiwemo ya vitendo vya uhalifu na inayafanyia kazi kwa mujibu wa sheria za nchi. 

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari na Wahariri wa vyombo vya Habari, ikiwa ni muendelezo wake wa kuzungumza na Waandishi kila mwisho mwa mwezi, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar 31, 12, 2022.

Rais Dkt.Hussein amejibu maswali ya Waandishi likiwemo linalohusu 'Video' inayotembea mitandaoni ikimuhusisha mwananchi wa Zanzibar aliyedai kufanyiwa vitendo vya kuteswa na vikosi vya SMZ.


Dkt. Mwinyi amejibu "Video mimi nimeiona. Watu wanalalamika, nataka kusema kuwa vyombo vya ulinzi vinaendelea kulinda raia na mali zao hivyo tupeni muda tunayafanyia kazi, yanachunguzwa na akibainika mtu wa ulinzi na usalama atachukuliwa hatua" amesema Rais Dkt Mwinyi.

Ameongeza kuwa Serikali inafuatilia suala la watu wanaojihusisha na vitendo vya kupiga na kupora watu maarufu 'Panya Road'  Zanzibar.


Wakati huohuo  Rais Dkt Mwinyi amempongeza mkuu wa mafunzo kwa hatua aliyoichukua ya kuwasimamisha kazi watumishi kadhaa baada ya wafungwa na mahabusu kutoroka.

Amesema kumekuwa na matukio ya kutoroka wafungwa na mahabusu hali ambayo inaleta wasiwasi kwa jamii visiwani hapo.



Rais Dkt Mwinyi amesema katika kupambana na suala la kuzuia vitendo vya unyanyasaji kwa watoto, ni kuhakikisha wanafunga mifumo thabiti,  kuwa na vifaa vya kisasa kama kipimo cha DNA.

"Ushahidi mzuri ni wa DNA,
hapa Zanzibar tunamashine tayari za DNA, hivyo ni kuwa na watu wenye ujuzi na weredi, vyombo vyetu vitafanya kazi nzuri" amesema Rais.




No comments