ONASTORIES YAWEZESHA VIJANA SHINDANO LA DUKUZI ZA KIBUNIFU
Na Andrew Chale, Dar es Salaam
KAMPUNI ya ONASTORIE imewezesha Wabunifu wa Kitanzania wakiwemo Wanafunzi wa Vyuo mbali mbali Nchini kushiriki kwa mara ya kwanza shindano la dukuzi za Kibunifu kwenye upande wa Teknolojia ya Uhalisia ongezi.
OnaStories wameendesha mafunzo hayo ya siku tatu yaliyofanyika ukumbi wa Dlab Kijitonyama Dar es Salaam kwa kushirikiana na wadau Kampuni ya META (zamani Facebook),IMISIED,Dlab na Blackrhino ambapo washindi walizawadiwa zawadi ikiwemo fedha za kusaidia bunifu zao.
Awali akizungumza katika mafunzo hayo, Mshirika mwenza wa kampuni hiyo,Tulanana Bohela amesema kuwa, mafunzo hayo ni kwa mara kwanza kufanyika nchini yakisimamiwa na OnaStories huku yakifanyika pia nchi zingine 16, ambapo washindi wa jumla watakutana pamoja kwa Bara la Afrika katika mafunzo makubwa zaidi hapo baadae.
"Tanzania ikiwa ni miongoni mwa Nchi 16 Barani Afrika ikiwa ni zaidi ya washiriki 1,000, OnaStories ikiwa ndio muendeshaji mkazi wa Udukuzi huo hapa nchini, imepata makundi kumi yaliyoshiriki kikamilifu ndani ya siku hizo tatu za kutafuta (kudukua) wazo tatuzi na lenye manufaa katika jamii ya Kitanzania". amesema Tulanana.
Amesema mawazo hayo yalijikita kwenye sekta ya elimu, afya, utalii, Biashara na ubunifu ambapo Udukuzi huo ukiwa ni muendelezo wa hatua ya awali ya Pre-Hackathon ambapo washiriki walikutanishwa na wataalamu kutoka pande zote za Afrika na kufundishwa mbinu mbalimbali na njia bora ya kutumia na kutengeneza wazo kupitia teknolojia za uhalisia ongezi.
Viongozi wenza wa kampuni ya OnaStories Bi. Tulanana Bohela (wa Kwanza kushoto) pamoja na wa Pili kulia Bw.Princely Glorious wakiwa pamoja na washindi, wakikabidhi mfano wa hundi ya zawadi kwa kundi bora la kwanza.
Washindi katika shindano hilo, kundi la kwanza walizawadiwa dola 1,500 USD na kupata nafasi kwenye mashindano makubwa zaidi ya Bootcamp yatakayoanza January hadi mwezi April, ambapo itakaribisha nchi 16 za Afrika.
Washindi wengine wakiwemo washindi wa pili walizawadiwa dola 800 huku mshindi wa tatu akipata dola 700. "Hii Bootcamp itakua Januari hadi April, Mshindi wa kwanza atapatiwa dola 10,000, wa pili dola 8,000 na watatu atapatiwa dola 7,000"amesema.
Viongozi wenza wa kampuni ya OnaStories Bi. Tulanana Bohela (wa Kwanza kushoto) pamoja na wa Pili kulia Bw.Princely Glorious wakiwa pamoja na washindi, wakikabidhi mfano wa hundi ya zawadi kwa kundi bora la kwanza.
Post a Comment