HEADER AD

HEADER AD

RHOBI AAHIDI USHIRIKIANO, CCM MWISENGE YASEMA NI MCHAPA KAZI


Na Jovina Massano, Musoma

MJUMBE wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania ( UWT ) Taifa katika Chama cha Mapinduzi (CCM), Rhobi Samwelly ambaye pia ni Mjumbe Kamati ya Siasa Mkoa wa Mara, amesema atashirikiana na Chama chake na Serikali kuanzia ngazi ya Kijiji na Mtaa kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo katika nyanja mbalimbali.

Rhobi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Hope for Girles and Women Tanzania, Akizungumza na Mwandishi wa DIMA Online, amesema kupitia nafasi yake aliyochaguliwa na wanachama atashirikiana na Chama chake katika kutekeleza Ilani ya CCM.

                       Rhobi Samwelly

"Katika nafasi hii nitashirikiana na Chama kuhakikisha tunatekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kuwaletea wananchi maendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwemo huduma za msingi za elimu,afya, maji safi na miundombinu.

"Lengo letu ni kuhakikisha tunaunga juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu za kuleta maendeleo kwa wananchi zinafanikiwa kwa asilimia 100.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)Kata ya Mwisenge Masere Majaliwa amempongeza Rhobi Samweli kwa nafasi aliyoipata pamoja na ahadi yake yenye mtazamo chanya kwa jamii.

               Mwenyekiti UWT Mwisenge

"Rhobi ni mwanamke mwenye uthubutu ni mpenda mabadiliko hivyo nafasi alizonazo naamini atazitendea haki, niwaombe wanachama wenzangu na wananchi kwa ujumla tuwe nae bega kwa bega ili kuuletea mkoa wetu Maendeleo.

 "Tuongeze ajira kwa wahitaji kwani miradi mbalimbali ikiongezeka kwenye maeneo yetu itahitaji nguvu kazi ambayo itatokana na wananchi wa eneo husika",amesema Masere.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Kata ya Mwisenge Mbogo Mnyugu amesema CCM inatekeleza Ilani yake ya kuwaletea maendeleo wananchi wake na viongozi waliopata ridhaa na kupewa nafasi zitumike kwa uwajibikaji.

               Mwenyekiti Kata ya Mwisenge akisalimiana na Rhobi Samwelly

"Akina mama ni Jeshi kubwa na Rhobi ni mwanamke mchapakazi mwenye uthubutu hakuna asiyejua hivyo, sisi tulio ngazi za chini tutahakikisha tunatoa ushirikiano wa kutosha kwa viongozi wetu ili malengo ya ilani ya Chama yatimie kwa watanzania wote kwani kaendeleo ndio hitaji la wananchi",amesema Mbogo.

         


No comments