VIONGOZI TPO WATAKIWA KUWA MFANO KWA JAMII
Na Scolastica Jackson, Tarime
VIONGOZI wa Shirika la Wazalendo Tanzania (TPO) wametakiwa kuwa wazalendo katika utendaji kazi ndani ya shirika na jamii inayowazunguka huku wakisisitizwa kuwaandaa vijana katika maadili mema ndani ya jamii ili kuwa mfano bora kwa Taifa.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Shirika la Wazalendo Mkoa wa Mara, Emmanuel Obombi Desemba, 9, 2022 wakati wa kikao cha kufunga mwaka kilichofanyika katika ukumbi wa hotel ya MT wilayani Tarime.
Emmanuel amewaonya viongozi kutojihusisha na mahusiano ya kimapenzi ndani ya shirika hilo na badala yake waheshimiane na kujenga jamii yenye maadili.
Mwenyekiti huyo amewaomba viongozi wa wilaya kuonesha ushirikiano na kutumia madaraka yao ipasavyo kuhakikisha palipo na tatizo panarekebishwa haraka lakini pia wawajengee vijana uwezo wenye uzalendo ili Taifa liwe na amani na vijana bora.
Afisa Mahusiano wa TPO Mkoa wa Mara Thobias Jackson amewaasa viongozi kuhakikisha wanakuwa na mahusiano mazuri na viongoz wa serikali pamoja na Taasisi mbalimbali katika wilaya walizopo.
Post a Comment