HEADER AD

HEADER AD

CCM SIMIYU: RAIS SAMIA NI MTEKELEZAJI WA ILANI, KATIBA


Na Mwandishi Wetu, Simiyu

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu Shamsa Mohammed amesema uamzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu wa kuruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa ni utekelezaji wa llani ya Chama cha Mapinduzi.

Kauli hiyo ameitoa Januari 4, 2023 wakati wa mkutano na Waandishi wa habari kufuatia Rais kuondoa katazo la mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa ambapo sasa ni ruksa kufanya mikutano ya kisiasa.

Shamsa amesema hatua hiyo ipo kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo Rais Samia ameonyesha kuisimamia sheria kikamilifu na kuilinda kama alivyo apa.

Amesema hatua hiyo inathibitisha kuwa nchi ina kiongozi anayetekeleza kiapo cha kikatiba, kiapo alichoapa kuisimamia katiba katika ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusimamia katiba na kuilinda.

"Amethibitisha kuwa tunaye kiongozi wa chama anayetekeleza ilani katika maeneo yetu, ameleta pesa nyingi za kimaendeleo katika mikoa yetu na ametekeleza demokrasia kama inavyoelekeza ilani ya ccm kwenda kuruhusu mikutano ya hadhara  kama inavyoelekeza ilani ya ccm ya mwaka 2020 ibara ya 110 kifungu kidogo 'c' ukurasa wa 161," Amesema Shamsa.

Amesema hatua hiyo inathibitisha kuwa anasimamia taifa zaidi ya chochote ndio maana ameruhusu kukosolewa kwa hoja na chama chochote au mtu yeyote kwa Iengo la kujenga taifa lenye umoja na kujenga jamii inayozungumza sauti moja yenye ustawi.

             Mwenyekiti CCM Simiyu

"Anathibitika kuwa ni kiongozi mwenye adhima yake ya kulikusanya taifa pamoja hivyo vyama vya upinzani vinatakiwa vijifunze hekima ya uongozi wa kidemocrasia  kutoka kwa Rais ili vitende kwenye vyama vyao kwa sababu vyama vingine vinaendeshwa kama makampuni binafsi na sio vyama vya kusimamia wanachama wao," amesema.

Hassan Msemakweli ni Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF) amesema wamepokea kwa shangwe na kuwa hiyo ni dalili tosha anataka Tanzania yenye umoja na mshikamano.

"Huu ni mwanzo tunakoenda ni vizuri kutoa fursa zaidi ili kuwe na democrasia ya kweli hasa katika masuala ya katiba pamoja na tume huru ya uchaguzi hivyo ni muda mzuri wa kumaliza matatizo ya watanzania," amesema Msemakweli.

Amesema viongozi wachukue  mfano katika nchi nyingine ambazo zinaiishi katiba na kusimamia haki ya kidemocrasia ili hata wapinzani tuuze sera kwa hoja za kutetea vyama vyetu.

"Tuwaombe viongozi upinzani tunapokwenda kwenye mikutano ya hadhara kujikita kwenye kujenga hoja kusema yale yote yanayopaswa kusemwa kwenye jamii" Amesema Msemakweli.

Ameongeza kwamba katika kukuza Democrasia zaidi ni lazima Rais ahakikishe mchakato wa katiba mpya unaharakishwa pamoja na tume huru ya uchaguzi.

No comments