HEADER AD

HEADER AD

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAKABILIANA NA MAJANGA


Na Mwandishi Wetu, Bariadi

JESHI la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Simiyu limesema kuwa kwa kipindi cha mwaka 2022 watu 43 wamekufa kwa ajali mbalimbali, ajali za majini na migodi zikiongoza kwa vifo vingi huku majeruhi wakiwa 114.

Akisoma taarifa ya Zimamoto na Uokoaji kwa kipindi cha  mwaka 2022, Kaimu Kamanda wa Jeshi hilo katika mkoa huo, Faustine Mtitu amesema hayo Januari 4, 2023, amesema Uokoaji uliofanyika umejumuisha ajali za migodini, kuzama katika madimbwi ya maji na ajali za moto.

         Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na ukoaji mkoa wa simiyu Faustine Mtitu 

Amesema wamekabiliana na matukio ya moto 21, uokoaji kwenye matukio 25 ikiwemo ajali za barabarani, migodi, mashimo ya vyoo, kusombwa na maji ya mvua, mabwawa na mito, matukio yaliyosababisha vifo vya watu 43, wanawake 29 wanamme 14 na majeruhi 114. 

Amesema majengo 1,537 na magari 76 yalikaguliwa maeneo 88 yalipatiwa elimu, wanufaika wakiwa ni watu 24,754, michoro ya majengo 26 ilisomwa na kupitishwa ikiwemo nyumba za kuishi 17, nyumba za biashara 05 na vituo vya mafuta 04 pamoja na kufanya vipindi 10 vya elimu kwa umma.


"Tunapouanza mwaka 2023 natoa wito kwa wananchi kufanya jitihada za makusudi kuhakikisha wanazuia majanga ya moto na kwa kuhakikisha maeneo yanafanyiwa ukaguzi wa tahadhari na kinga dhidi ya majanga ya moto ili kuondoa uwezekano wa kutokea matukio ya moto kwenye maeneo yao," amesema Mtitu.

Amewataka wananchi kuhakikisha kila mmoja anakuwa na walau kizima moto cha awali (Portable Fire Extinguisher) pamoja kuhakikisha wanapatiwa elimu ya tahadhari na kinga dhidi ya majanga ya moto na majanga mengine kwenye maeneo ya kazi.



Ameongeza kusema kuwa matukio yaliyovuta hisia za wananchi ni pamoja na ajali ya gari iliyotokea eneo la Nyamikoma Wilaya Busega Januari 11, 2022 lililosababisha vifo vya watu 15.

Ajali nyingine ni ile ya gari ilitokea eneo la Kidurya Wilaya ya Bariadi  Machi 27, 2022 iliyosababisha vifo vya watu 07 na tukio la moto wa nyumba ya ndugu Edward Sabato mtaa wa mji wa zamani Bariadi lililotokea Agosti 08, 2022.







No comments