HEADER AD

HEADER AD

GARI LAFIKA NA VITANDA, MAGODORO KISHA LAONDOKA NAVYO


Na DIMA Online, Tarime

WANAKIJIJI cha Bisarwi Kata ya Manga Wilaya ya Tarime mkoa wa Mara wanaendelea kusubiri vitanda na magodoro vilivyofikishwa katika Zahanati ya Kijiji hicho vikiwa ndani ya gari kisha gari kuondoka navyo.

Gari la Halmashauri ya Wilaya ya Tarime lilifika kijijini hapo Januari, 11,2023 likiwa limebeba magodoro na vitanda vilivyotakiwa kuwekwa ndani ya Zahanati ya Bisarwi ambayo bado haijaanza kutoa huduma. 

Kwa mujibu wa wanakijiji wanasema  majira ya saa tisa alasiri yalifika magari mawili katika Zahanati hiyo moja likiwa limebeba vitanda na magodoro ya Zahanati na gari lingine likiwa na Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara.

Imeelezwa kuwa baada ya kufika katika Zahanati hiyo siku ambayo ni ya mnada katika Kata hiyo walikuta mlango wa Zahanati umefungwa na hivyo kuondoka na vifaa hivyo.

                  Zahanati ya Bisarwi

Imedaiwa kuwa uongozi wa Kijiji haukuwa na taarifa ya ujio wa mbunge na vifaa hivyo kwamba walifika kwa kushtukiza ambapo muhusika anayekaa na funguo hakuwepo karibu na hakuwa na taarifa yoyote ya ujio huo.

Hata hivyo wakati magodoro na vitanda vimefikishwa katika Zahanati hiyo kwa kusindikizwa na Mbunge Waitara kulikuwa na muuguzi mmoja na mjumbe wa Serikali ya Kijiji.



No comments