WAPEWA ELIMU YA BIMA YA AFYA KWA WOTE
Na. WAF - Mwanza
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imewajengea uelewa kuhusu Bima ya Afya kwa wote viongozi wa makundi ya Wamachinga, Wakulima, Wavuvi, Wachimba Madini, Bodaboda, Mama Lishe na Kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza ili wakawe Mabalozi wa kutoa elimu ya Bima ya Afya.
Akitoa elimu ya Bima ya Afya kwa wote kwa makundi hayo Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi amesema lengo ni kila mwananchi kwa hali yake aingie Kwenye mfumo wa Bima ya Afya.
Ameeleza kuwa Muswada wa Bima ya Afya kwa wote ukipitishwa utaongeza wigo wa wananchi wengi kujiunga katika mfumo wa Bima ya Afya kutoka asilimia 15 ya sasa mpaka asilimia zaidi ya 90 na kuendelea ya Watanzania.
“Serikali makini haiwezi kuacha makundi yote haya muhimu wabaki bila kuwa na uhakika wa matibabu ya afya zao, lazima kuweka mpango wa Bima ya Afya kwa wote ambapo mtu akiugua kwa hali yoyote ya kifedha aliyonayo aweze kutibiwa kwa haraka na wakati ili aendelee na shughuli zake za utafutaji" amengeza Prof. Makubi.
Post a Comment