HEADER AD

HEADER AD

KITUO CHA MAKUMBUSHO CHAPOKEA WAGENI ZAIDI YA 300


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KITUO cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kimepokea wageni zaidi ya 300 ambao ni viongozi wa shirika lisilo la kiserikali la Utold Foundation kutoka nchi mbalimbali Afrika Mashariki na nje ya Afrika Mashariki. 

Imeelezwa kuwa imekuwa ni utaratibu wao wa kutembelea nchi mbalimbali ambazo Shirika hilo lina matawi yake na awamu hii ilikuwa Tanzania.


Safari hiyo imeandaliwa na viongozi hao kutembelea vituo vya utalii vinavyopatikana Dar es Salaam na moja ya kituo walichotembelea ni Makumbusho ya Taifa la Tanzania, na Nyumba ya Utamaduni.

Mratibu wa safari hiyo ndugu Donald Mbeke amesema " Tuliona Makumbusho ya Taifa ni sehemu sahihi kuwaleta wageni wetu ili waweze kujifunza juu ya Masuala ya uongozi, historia ya nchi yetu na utamaduni wetu". 


"Ni muda sana sijafika hapa Makumbusho ya Taifa nimekuta mambo yamebadilika sana natoa shukrani kwa uongozi wa Makumbusho ya Taifa kwa ujumla namna walivyowapokea na kuwapatia huduma rafiki kwa kila mmoja na kuahidi kurudi kwa awamu ya pili. 

Afisa Elimu Mwandamizi wa Makumbusho ya Taifa Anamery Bagenyi amemshukuru Mratibu wa safari hiyo kwa kuona Makumbusho ya Taifa ni sehemu sahihi ya kutembelea na kujifunza.

Ametoa wito kwa Mashirika mengine ya kiserikali na yasio ya kiserikali kuiga mfano wa shirika hilo la Utold Foundation kwani makumbusho ni sehemu sahihi sana kwa kujifunza historia ya nchi na kuna kumbi ambazo wanaweza kufanyia mikutano mbalimbali.



No comments