HEADER AD

HEADER AD

MZEE WA POINT 3 ANADI SERA ZAKE, AWAOMBA WANACHAMA WAMCHAGUE

 


Na Andrew Chale, Dar es Salaam

INJINIA Rashid Khamsini anayegombea nafasi ya ujumbe wa Bodi ya Ukurugenzi katika Uchaguzi Mkuu wa Simba, amewaomba wanachama kumchagua ilikuwatimizia lengo la ushindi na kuchukua mataji ya ubingwa.

Akiendelea kunadi sera zake kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Simba Januari 29, katika ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam, Eng. Khamsini amesema atakuwa kiunganishi muhimu cha wanachama mwekezaji na wadau wa soka nchini na nje ya nchi huku akitumia kauli mbiu ya pointi tatu kila mechi.

"POINT3' kila mechi ni mkakati wa kisera ambapo mimi mjumbe wa bodi napochaguliwa lazima tuitungie sera iwe inafanyika kivitendo na sio maneno ya porojo.

           Mgombea ujumbe wa Bodi

"Lazima tuwe na muunganiko wa viongozi na wanachama (simba nguvu moja maanake ni hii kauli) wanachama wa simba na viongozi tukiungana ndo tutaweza kuirejesha nguvu ya timu na kushinda kila mechi."amesema Eng.Khamsini.

Lazima tuwe na 'scouting' ya uhakika hapo nazungumzia simba sc lazima iajili seasoned technical director (mbobezi kabisa kwenye kwenye sector Hiyo mkurugenzi wa ufundi ndo kiungo cha club)

Amesema Simba lazima iwe benchi la ufundi lililokuwa na wakufunzi waliobobea kwenye eneo hilo, lengo kuu ni kuweza kuwapa mafunzo mazuri wachezaji na pia kuiendeleza na Simba B iweze kuzalisha wachezaji simba kubwa.

Ameongeza kuwa itasaidia kupunguza gharama za usajili na pia itaongeza kipato klabu kwa kuuza na pia hata itakuwa chanzo kizuri kwenye timu yetu ya taifa.

"Muunganiko wa hayo machache matatu ndo msingi wa POINT3 kila mechi na silaha zengine za vita nimezificha zipo za kutosha kabisa.

Amesema kubwa kabisa Simba bila kumfunga yanga aina maana yoyote ili simba sc wanachama tufurahi lazima wawafunge yanga kuanzia mechi ya mwezi wa 4 na kwamba wanachama wakimchagua basi yanga atafungwa magoli ya kutosha. 

"Lazima tusimame na vision ya mwekezaji na wanachama wote tuchukue kombe la Africa na Hiyo yote inawezekana iwapo wanachama wa simba watanipa ridha na kunichagua kuwa mjumbe wa bodi.

"Naombeni KURA zenu mnipigie kwa kishindo siku ya uchaguzi 29-01-2023. Nitumeni kazi kwa kukupigia KURA kwa wingi." Amesema Eng Rashid 

Mgombea huyo hadi sasa ameweza kutembelea matawi mbalimbali ya Simba ikiwemo Dar es Salaam na Mikoani na kunadi sera zake.

No comments