HEADER AD

HEADER AD

WAKILI MOSES KALUWA: MKINICHAGUA NITABUNI MIRADI KUIONGEZEA MAPATO SIMBA SC




Na Andrew Chale, Dar es salaam

WAKILI msomi na Mwanasheria, Moses Kaluwa anayegombea nafasi ya uenyekiti Simba SC amenadi sera zake katika matawi mbalimbali zaidi ya 30, ikiwemo Jijini Dar es Salaam na Mikoani ikiwa ni hatua ya mwisho kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Simba Januari 29 utakaofanyika ukumbi wa JNICC.

Akiwa katika mwendelezo wa kampeni hizo mapema Januari 27, katika matawi ya Dar es salaam, ameweza kukutana na  matawi zaidi ya Sita (6) ya Wanachama wa Simba yakiwemo ya Simba Dume la Mwembe chai, Wekundu wa Terminal (Mbezi mwisho), Vuvuzela la Mwananyamala, Mdomo wa Simba na mengineyo.

Kaluwa katika kampeni hizo amenadi vipaumbele vyake mbalimbali huku akiahidi kushirikiana na viongozi wengine pamoja na Mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji Mo, na Wanachama wote wa Simba nchi nzima na nje ya nchi.

      Wakili na Mwanasheria, Moses Kaluwa anayegombea nafasi ya uenyekiti Simba SC.

"Vipaumbele vyangu ni pamoja na kushirikiana na matawi yote nchi nzima, kuhakikisha kila mwanachama mwenye vigezo anapata uwanachama Kwa mujibu wa taratibu, lakini pia kubuni miradi kwa kushirikiana na Mwekezaji na wadhamini wa ndani na nje.

"Kuhakikisha bodi inakuwa na uendelezaji wa miundombinu ya viwanja vya mazoezi na mechi.
Lakini kuwa na kuendeleza miradi ya vipaji vya Watoto na vijana, kujenga mbinu za kuongeza hamasa, kuajiri watalaam wa kila eneo ilikuwezesha timu kupata matokeo." Amesema Kaluwa.

Aidha ameongeza kuwa katika vipaumbele vyake hivyo ni kuhakikisha Simba inaongeza mapato, kujenga tamaduni imara.


" Nitahakikisha tunadumisha mila, desturi na tamaduni zilizoasisiwa na Wazee wetu ambao ni waanzilishi wa klabu na ambazo tumedhirithi zinaenziwa na kulindwa kwa ajili ya vizazi vijavyo" amesema Kaluwa.

Amesema atahakikisha anajenga, kuyalinda, na kuyaenzi mahusiano mazuri yaliyopo  kati ya mashabiki, Wanachama, Mwekezaji na wadhamini kwa kila eneo kwa Maendeleo ya Simba.

Wagombea wengine ambao wameweza kuungana kunadi sera ni pamoja na Eng Rashid Mashaka ambaye ni mgombea wa Ujumbe Bodi ya Ukurugenzi.

Kaluwa ananadiwa na Mwenyekiti wa zamani, Hassan Dalali na wanachama wa Simba wa matawi mbalimbali.




No comments