HEADER AD

HEADER AD

HAYA NDIO MASWALI YA MWANDISHI YALIYOHITAJI MAJIBU YA MKURUGENZI TARIME MJI


>>>Mkurugenzi wa Halmashauri hakujibu na alikataa kuhojiwa

>>>Huku akisema Mwandishi ni mganga njaa,mbabaishaji.

Na Mwandishi Wetu, Tarime

MWANDISHI wa Habari anaye ripotia Chombo cha Habari cha Mtandaoni DIMA Online, Dinna Maningo Februari,2, 2023 alifika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Tarime Mkoani Mara, Gimbana Ntavyo kutaka ufatanuzi wa habari aliyokuwa akiifuatilia.

Mwandishi alikuwa anafuatilia habari kufahamu mafanikio na changamoto za elimu katika shule ya msingi Magufuli ya Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum ambao ni wanafunzi wenye ulemavu wa akili, wasioona na wasiosikia iliyopo Kata ya Nyamisangura katika Halmashauri hiyo lakini hakujibiwa chochote zaidi ya kutolewa maneno makali na Mkurugenzi huyo juu ya habari aliyoiandika mwezi mmoja uliotipa.

Mkurugenzi huyo alikataa kuhojiwa na kusema mwandishi huyo ni mganga njaa, mbabaishaji kwamba aliandika habari na kupiga picha za uongo za ujenzi wa vyumba vya madarasa habari iliyoripotiwa DIMA Online Desemba, 19,2022 licha ya kwamba mwandishi alifika kwenye maeneo husika kushuhudia ujenzi na kupiga picha za madarasa yakiwa hatua mbalimbali za ujenzi.

Shule ya msingi Magufuli awali wanafunzi wenye ulemavu wa akili, wasioona na wenye ulemavu wa kusikia walisoma kwa kuchangia darasa moja katika shule ya msingi ya Turwa yenye kitengo cha elimu maalum kwa wanafunzi wenye ulemavu kabla ya kuhamishiwa kwenye shule mpya ya Magufuli;

Serikali katika kuhakikisha inaboresha mazingira mazuri ya wanafunzi kujifunzia ikajenga shule mpya nyingine  ya msingi maalum kwa wanafunzi wenye ulemavu iliyopewa jina la Magufuli ambayo hivi karibuni inatarajiwa  kusajiriwa.

Maswali

 Je ni kwa namna gani Serikali imefanikiwa kuboresha mazingira rafiki ya elimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum ikiwemo miundombinu ya ujenzi?

2 Kwakuwa shule hiyo imejengwa kwa fedha za Serikali Je ni kiasi gani cha fedha kilichogharimu ujenzi.

          Shule ya msingi Magufuli ya Wanafunzi wenye Mahitaji maalum

3. Serikali imekuwa ikigharamia huduma zote bure bila mzazi kuchangishwa chochote, je Serikali uchangia kiasi gani cha fedha katika huduma ya chakula katika shule hiyo?

4.Serikali imekuwa ikijitahidi kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira rafiki na walimu wanafundisha katika mazingira rafiki, Je kwa namna gani Serikali imefanikiwa kupeleka shuleni vitendea kazi vya kujifunzia na kufundisha.

5.Mwaka 2019 shule ilisajili wanafunzi wenye ulemavu wa kuona lakini hadi sasa haijawahi kuwa na vitabu vya kujifunzia vya Nukta Nundu je ni lini itapata vitabu na kwanini mpaka sasa haijawahi kupata vitabu?

6.Shule ina mashine moja ya kuchapa maandishi kwa ajili ya wanafunzi wasioona kujifunza, wanafunzi na walimu wanalazimika kuchangia mashine moja je ni lini shule itapata Mashine zingine ili kuweka mazingira rafiki ya kujifunzia na kufundishia ?

7.Shule haina kamusi ya lugha za alama tangu kitengo kilipoanzishwa mwaka 2012, je ni kwanini hazipo na lini shule itapata kamusi hizo?

8.Shule haina walimu wa darasa la awali  hadi la pili walimu waliopo wa madarasa ya juu ndio wanao wafundisha, je nini sababu ya ukosefu wa walimu hao na lini shule itapata walimu?

9. Shule haina vyoo vya walimu wanalazimika kutumia vyoo vya wanafunzi, je ni lini watajengewa vyoo vyao?

10.Shule haina Bendera ya Taifa wala kibao cha Shule je kwanini havijawekwa na vitawekwa lini?

11.Shule haina ofisi ya walimu ( Staff) wanatumia darasa, je ni lini watapata Ofisi?.

12.Shule haina vifaa vya kufundishia somo la Sayansi kwa wanafunzi wasioona darasa la 5-7, je ni lini vitabu vitapelekwa n kwanini havipo?

13.Shule inahitaji kuwa na mtaalam wa tiba mazoezi na Tiba matamshi, je nini mkakati wa Halmashauri na Idara ya Elimu kuhakikisha inapata wataalam hao?

14.Je Majengo ya Shule, choo, bweni ujenzi wake umegharimu Sh. Ngapi?

15. Baadhi ya waafunzi wamekatisha masomo ambapo sababu ni wazazi kukosa gharama za nauli kupeleka wanafunzi shuleni, Serikali imejega Bweni moja kwa ajili ya wasichana je  litakamilika lini?
           Bweni la Wasichana ambalo bado halijakamilika ili wanafunzi walitumie

16. Je jinsia nyingine ya kiume wao watajengewa lini bweni kama njia ya kuwasaidia wanafunzi kuishi shuleni ili wasikatishe masomo kwa kukosa nauli ya usafiri wa kwenda shule?

Hata hivyo maswali hayo hayakufanikiwa kupata majibu bada ya Mkurugenzi huyo kugoma kuhojiwa huku akimpiga marufuku mwandishi kufika ofisini kwake.

Mwandishi huyo alifika ofisi ya Mkurugenzi baada ya afisa Elimu Msingi katika Halmashauri hiyo John Matiko Kebaha kukataa kuzungumza na kumtaka Mwandishi huyo kwenda kuomba kibali kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ndipo wazungumze.

"Nipo Tayari kuzungumza na wewe lakini naomba uende kwa Mkurugenzi akupe kibali kisha uje tuzungumze, kuna Mwandishi wa Habari aliwahi kuripoti habari bila kibali cha Mkurugenzi aliyekuwepo kwa wakati huo ilituletea shida sana naomba uende kwa Mkurugenzi uzungumze nae" alisema Matiko. 

>>>Desemba, 18, 2022 Mwandishi huyo wa habari alitembelea baadhi ya shule kuona hali ya ujenzi unavyoendelea ambapo Desemba, 19,2022 aliripoti Habari yenye kichwa cha habari kisemacho 'TARIME TC YASHINDWA KUTEKELEZA AGIZO LA NAIBU WAZIRI TAMISEMI' ikiwa na picha za ujenzi wa vyumba vya madarasa habari ambayo imeonekana kumchukiza Mkurugenzi huyo wa Halmashauri akidai ni habari ya uongo.

No comments