HEADER AD

HEADER AD

WADAU WAJADILI MFUMO SHIRIKISHI WA AFYA KIDIGITALI 'AFYA SS'

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WIZARA ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa pamoja na wadau wake wakiwemo PATH Tanzania, wamekutana Jijini Dar es Salaam kujadili namna bora ya matumizi ya mfumo wa kidigitali wa Afya Supportive Supervision (AFYA SS) ilikurahisisha mfumo bora wa kisasa na kuachana na matumizi ya makaratasi.

Akizungumza katika kikao hicho, Mratibu wa mafunzo hayo ya siku moja, kutoka idara ya  'Quality insurance' kitengo cha usimamizi shirikishi katika Wizara ya Afya, Dkt.Chrisogone German amesema kuwa wadau hao wamejifunza mambo mbalimbali lengo likiwa ni kuboresha huduma bora za Afya kidigitali.

       Mratibu wa mafunzo ya siku moja juu ya kujadili namna bora ya matumizi ya mfumo wa kidigitali wa Afya Supportive Supervision (AFYA SS), kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Chrisogone German akiwasilisha mada katika  kikao hicho

"Mfumo wa kidigitali wa supervion, ni mfumo ambao umetengenezwa kwa maana kushirikiana na ofisi ya Rais TAMISEMI na wadau mbali mbali wakiwemo PATH Tanzania kupitia mradi wao wa 'Data Use Partnership' (DUP) ili tuweze kuwa na mfumo ambao utarahisisha suala la usimamizi shirikishi na kuachana na matumizi ya makaratasi. Ameeleza Dkt. Christogone German.

Aidha, amesema wameweza kupitia masuala tofauti tofauti ya mfumo ili kuona namna bora ya kuendeleza.


"Wadau zaidi ya 30 wameweza kushiriki mkutano huo pamoja na wengine kushiriki kwa njia mtandao, pia wameweza kutoa maoni na namna bora ya kuendeleza mfumo huu."Amesema Dkt Chrisogone.

Katika mkutano huo, Wadau hao wakiwemo Madaktari, Watalaam wa Taasisi za ndani na nje ikwemo AMREF, PATH Tanzania, Chuo Kikuu Mzumbe, TAMISEMI na wengine walichangia mawazo yao katika kufanikisha maendeleo yake.

       Mkurugenzi wa Mradi wa Data Use Patnership (DUP) kutoka PATH Tanzania, Dkt. Seif Rashid akizungumza katika kikao hicho.




No comments