HEADER AD

HEADER AD

UTATUZI KWA NJIA YA USULUHISHI UTAOKOA GHARAMA KWA WANANCHI

 

Na Jovina Massano, Musoma

IMEELEZWA kuwa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi ni kuokoa muda na gharama wanazozitumia wananchi kutafuta mawakili pindi wanapokuwa na mashauri mahakamani na badala yake watazitumia katika kukuza shughuli zao za kiuchumi.

Kauli hiyo imetolewa Februari, 01, 2023 na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, Fahamu Mtulya alipokuwa akihitimisha wiki ya sheria mkoani hapo.

       Jaji Mfawidhi Mahakama kuu Kanda ya Musoma Fahamu Mtulya

Amesema huo ni utekelezaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha 107 A ,(1) na (2) kinataja moja kwa moja mahakama na mambo ya usuluhishi.

Amesema katiba haijatenganisha aina ya usuluhishi bali imesema wadaawa pande zinazoleta shauri mahakamani wafurahie usuluhishi.
Waalikwa kutoka taasisi mbalimbali

"Mfano amri ya 8 yenye kipengele A,B na C ya Sheria ya mwenendo wa taratibu za madai(Civil Procedure Court) sura namba 33 inaruhusu madai yoyote yanayohusu mtu na mtu au kampuni kwa kampuni kupitia njia ya usuluhishi bila kujali ukubwa au Mamlaka ya shauri husika tofauti na jinai", Amesema Mtulya.

Mgeni wa heshima katika kilele hicho cha wiki ya sheria Mkuu wa wilaya ya Butiama  Mwl.Moses Kaegelle akimwakilisha mkuu wa mkoa Meja Jenerali Suleiman Mzee alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan na Serikali kwa kazi kubwa ya kulinda na kusimamia amani ya Taifa.

       Mwl.Moses Kaegelle mkuu wa wilaya ya Butiama

Amesema Rais amewezesha mpango mkakati wa huduma za mahakama  ambapo mkoa umepata mahakama mbili mpya katika wilaya ya Butiama na Rorya ili kusaidia wananchi kupata huduma karibu.

Ameongeza kuwa katika maadhimisho hayo kauli mbiu ni 'Umuhimu wa Utatuzi wa  Migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu wajibu wa mahakama na wadau' inatakiwa suala la suluhu hivyo liungwe mkono na wadau wote kwani wilayani Butiama migogoro ya mipaka ipo mingi.

Makalani wa Mahakama

"Kusiwe na usuluhishi kwenye mashauri ya ubakaji, ulawiti, ukeketaji na mimba za utotoni adhabu itolewe ili kudumisha amani na kulinda usawa, lakini pia amewaomba viongozi wa dini kuhubili amani na kuwaasa waumini kupinga vitendo vya ukatili kwani hivi sasa wimbi la ukatili limeongezeka.

Wakati huohuo, Askofu wa Jimbo Kuu Katoriki Musoma Michael Msonganzila amesisitiza kuwa usuluhishi uangaliwe kulingana na shauri kama ni la jinai liangaliwe lisiwe na madhara ili kuwe na usalama katika jamii.

       Askofu wa Jimbo Katoriki Musoma Michael Msonganzila

"Makosa ya usuluhishi na upatanisho nje ya mahakama yaangaliwe yasiwe ya ukatili, ugaidi na utumiaji wa dawa za kulevya yawe ya kawaida kama Migogoro ya ndoa, majirani kwa majirani, makosa mazito yaangaliwe sana kwa umakini mkubwa ili yasilete madhara kwa jamii"Amesema Askofu.

Maria Julius Kimario mkazi wa barabara ya  Sokoine Kata ya Mwigobelo ameipongeza mahakama kwa kuanza kufanya usuluhishi wa mashauri nje ya mahakama lakini wazingatie aina ya mashauri ambayo watafanya upatanisho huo na kuzingatia haki na usawa kwa wadau.

          Maria Julius Kimario
              
           Mahakimu wa Mahakama


      Wananchi waliohudhulia kilele Cha sheria




      

No comments