HECHE : MARUFUKU MICHANGO TARIME VIJIJINI
>>>Asema Halmashauri ya Vijijini ina fedha nyingi
>>>Ampiga Marufuku Ded kudhulumu wananchi
>>>Asema ataruka na Halmashauri kama mwewe
Na Dinna Maningo, Tarime
Ameongeza kusema "Mimi kwenye uongozi wangu tulijenga madarasa 16,500 hatukuchangisha wananchi hata Tsh. 100, sasa leo fedha zote hizo unaambiwa uchange, hata choo kikianguka unaambiwa uchange, mimi nachotaka watoto waende shule choo kimeanguka hiyo ni kazi yao.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Mara, Lucus Ngoto ameunga mkono kauli ya John Heche na kusema ni marufuku Jimbo la Tarime Vijijini wananchi kuchangishwa fedha.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na aliwahi kuwa mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini mwaka 2015-2020, John Heche amepiga marufuku wananchi wa Jimbo la Tarime Vijijini kuchanga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Amepiga Marufuku hiyo wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na chama hicho Februari,17,2023 uliofanyika Kijiji cha Kegonga Kata ya Nyanungu na Kijiji cha Nyamwaga Kata ya Nyamwaga Jimbo la Tarime Vijijini.
Akiwa katika Kijiji cha Kegonga John amesema kuwa haoni sababu ya wananchi wa jimbo hilo kuchangishwa michango hili hali halmashauri hiyo ina fedha nyingi zitokanazo na mapato ya ndani.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Heche akizungumza na wananchi wa Kata ya Nyanungu
Amesema fedha hizo ni pamoja na fedha za ushuru wa huduma, fedha za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) na fedha kutoka Serikali kuu zinazotolewa kutekeleza miradi ya maendeleo.
"Wananchi ni marufuku kutoa michango halmashauri imepata fedha kutoka mgodini zaidi ya Tsh.Bilioni 10 ni marufuku wananchi kuchanga kitu chochote, mtu akija kwako Mwenyekiti wa Kijiji au mtu mwingine hakuna kuchanga.
"Nimekataa nasema mbele ya Polisi nimepiga marufuku kuchanga michango , mkisema Heche anagomesha semeni, haturuhusu wananchi kuchanga kwasababu halmashauri yetu ina fedha tunataka madarasa yajengwe.
"Wewe unachotakiwa ni kununua sare za shule na madaftari mtoto aende shule, wanachangisha wananchi fedha alafu zinainga kwenye matumbo yao" amesema Heche.
Akiwa katika Kijiji cha Nyamwaga John amesema alipokuwa mbunge wa jimbo hilo na halmashauri ya wilaya ya Tarime kuongozwa na CHADEMA wananchi hawakuchangishwa fedha licha ya kwamba ilikuwa na mapato kidogo ikilinganishwa na sasa inavyoongozwa na Chama cha Mapinduzi (CCM).
" Halmashauri imepata mapato ya ndani ya mgodi fedha za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) zaidi ya Bilioni 7 bado hujaweka na makusanyo mengine lakini bado inachangisha michango wananchi.
"Halmashauri ilipoongozwa na CHADEMA haikuchangisha wananchi michango, tulikuwa na mapato Tsh. Bilioni 1.7 lakini tukajenga vituo vya afya 9 kikiwemo kituo cha afya Sirari, Nyarwana, Muriba, hapa Nyamwaga na Kerende.
Ameongeza kusema "Mimi kwenye uongozi wangu tulijenga madarasa 16,500 hatukuchangisha wananchi hata Tsh. 100, sasa leo fedha zote hizo unaambiwa uchange, hata choo kikianguka unaambiwa uchange, mimi nachotaka watoto waende shule choo kimeanguka hiyo ni kazi yao.
"Tuliongoza halmashauri bila michango na aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri Moses Misiwa alijitahidi sana kusimamia miradi, atarudi CHADEMA na akirudi mumpokee, alafu anakuja mtu anasema maendeleo maendeleo, hata hii Hospitali ya halmashauri imejengwa wakati wa uongozi wetu"amesema Heche.
Ampiga marufuku Ded kudhulumu
John amesema ni marufuku Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya wilaya ya Tarime Solomon Shati kudhulumu wananchi kisa kujenga stendi na kwamba wananchi wote wanapaswa kulipwa fidia huku akiahidi kufuatilia kwa ukaribu matumizi ya fedha za miradi katika Halmashauri hiyo.
"Mkurugenzi ni marufuku kudhulumu wananchi eti kisa unajenga stendi wote walipwe fidia kwasababu halmashauri ina hela.Wasiwatishe hapa eti wanawaambia mkidai fidia halmashauri haitajengwa itajengwa, halmashauri haiwezi kuondoka ilishaletwa Nyamwaga kinachofanyika ni upanuzi wa mji tutapanua na utakuwa mji unaostahili.
"Wale wanaodai fidia yao Mkurugenzi unaijua sheria ya ardhi, wakati tunajenga hii Hospitali ya halmashauri kulikuwa na watu pale tulilipa fidia watu na wakati ule mapato yetu ya ndani kutoka Mgodini yalikuwa Bilioni 1.7 leo halmshauri hii imepata zaidi ya Bilioni 7 bado inachangisha" amesema John.
Amesema atahakikisha anafuatilia kujua namna fedha za miradi itokanayo na mapato ya ndani zinavyotekelezwa na kwamba kazi ya Serikali ni kufanya maendeleo na si hisani hivyo rasilimali za Taifa zitumike kwa maendeleo.
"Mkurugenzi fedha zitumike vizuri unakaa na madiwani mnaiba hela mtazitapika, nataka kuruka na nyie kama mwewe, si mlikuwa mnajitawala, mnaibia wanachi alafu mnarudi kuwaambia michango michango.
"Hakuna michango kuanzia leo mwananchi wakikudai michango hakuna kuchanga na nimesema Polisi wapo hapa wanasikia michango nidaini mimi, wananchi wote kuanzia leo wapo huru kutochangia fedha nunua sukari uweke kwenye uji watoto wanywe, kazi ya Serikali ni kufanya maendeleo rasilimali zetu zinufaishe zitumike kwa maendeleo" amesema John.
Aliyewahi kuwa Katibu wa John Heche alipokuwa Mbunge ambaye kwa sasa ni Katibu wa Kamati ya sheria na haki za Binadamu Kanda ya Serengeti CHADEMA, Mrimi Zabron amesema wakati John akiwa mbunge wananchi hawakuchangishwa fedha za miradi ya maendeleo licha ya kuwa na makusanyo kidogo na miradi mingi ilijengwa kama barabara, madarasa na huduma za afya.
Amesema kuwa kwa sasa Serikali imetoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo zikiwemo na fedha za mapato ya ndani kutoka mgodi wa Dhahabu wa North Mara za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) zilizoongezeka lakini bado wananchi wanachangishwa fedha.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Mara, Lucus Ngoto ameunga mkono kauli ya John Heche na kusema ni marufuku Jimbo la Tarime Vijijini wananchi kuchangishwa fedha.
"Mimi kama kiongozi wa Chama naunga mkono kauli hilo, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime haina sababu hata moja ya kuomba wanachi michango, habari za watu kukamatiwa sufuria, kuku, mbuzi kisa michango kwasababu ya kujenga choo , madarasa wakati huo Serikali imeleta fedha nyingi na inakusanya mapato hatutakubali.
"Tumekuwa na halmashauri ambayo huwezi kusikia wala kujua nini kinaendelea katika halmashauri, tumekuwa na madiwani ambao hawawezi kutetea wananchi, kuna Diwani mmoja wa Kata ya Nyanungu alijitokeza kutetea wananchi akawekwa ndani kituo cha Polisi.
Lucus amesema kuwa halmashauri zimekuwa zikitegemea fedha za miradi ya maendeleo kutoka Serikali kuu huku fedha za mapato ya ndani hazijulikani zimefanya kazi gani na hivyo kudai huwenda zinatafunwa.
"Tumemsikia Waziri Mkuu akilalamika na kuzungumza kwamba vyanzo vya mapto ya ndani katika halmshauri nchini havitekelezi maendeleo ipasavyo wanasubiri pesa kutoka Serikali kuu ,zikiwemo fedha za UVIKO.
"Mabilioni yanatoka mgodini watu wanagawana, makusanyo wanakusanya yanaishia kwenye matumbo ya watu, Madiwani walikuwa wanafanya utumbo na ujinga kwasababu tulikuwa hatuna uwezo wa kuwaambia wananchi.
" Sasa tutazungumza na wananchi tutawaambia viwango vya fedha vinavyotolewa mgodini Diwani aje haitishe mkutano atuambie fedha za mapato ya ndani zimetekeleza miradi gani" amesema Lucus.
Ameitaka halmashauri na madiwani kusimamia vizuri matumizi ya fedha za miradi ili ifanye maendeleo ya wananchi na sio wananchi kuchangishwa fedha bila sababu za msingi hili hali halmashauri ina fedha nyingi za CSR.
Post a Comment