HEADER AD

HEADER AD

MTUHUMIWA WA MAUAJI AKAMATWA BAADA YA KUPATA NJAA MAFICHONI


>>>Ni baada ya kupata njaa na kwenda kuomba chakula

>>>Anatuhumiwa kumuua mmoja wa familia alikokua akiishi

>>>Polisi wamuhoji ili kukamilisha upepelezi


Na Alodia Babara, Bukoba

HATIMAYE Jeshi la Polisi mkoani Kagera limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa mauwaji Paschal Kaigwa Marisel mkazi wa kata ya Rwamishenye- Bukoba anayedaiwa kufanya mauwaji na kutokomea kusikojulikana kwa siku takribani sita akikwepa mkono wa sheria.

Mtuhumiwa huyo ni Paschal Kaigwa Marisel (21) mkazi wa Mtaa wa National housing kata ya Rwamishenye manispaa ya Bukoba anayetuhumiwa kwa mauaji ya Hadija Ismail (29).

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera Wiliam Mwampaghale amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kusema kuwa wanaendelea kumuhoji ili jeshi hilo liweze kukamilisha upepelezi kwa ajili ya kumfikisha mtuhumiwa mahakamani.

     Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera Wiliam Mwampaghale

Kamanda William amesema mtuhumiwa amekamatwa  Februari,19, 2023 baada ya kutoka mafichoni alikokuwa amejificha kutokana na kuumwa njaa na kwenda kuomba msaada wa chakula nyumbani kwa shangazi yake mtaa wa kashai Katotorwansi manispaa ya Bukoba.

 “Mtuhumiwa wa mauji ya Hadija Ismail tumemkamata Februari 19,2023 majira ya saa 10:00 jioni baada ya kutekeleza mauji Februari 13,2023 na kwenda kujificha katika vichaka kwa muda wote huo.

" Baada ya njaa kali aliamua kutoka mafichoni kwenda kwa shanghazi yake kuomba chakula alipofika nyumbani shanghazi yake hakuwepo walikuwepo watoto waliokuwa wanamfahamu ambao baada ya kumuona walipiga kelele na majirani wakafika na kumkamata” Amesema Mwampaghale.

Ameongeza" Ikumbukwe kuwa kijana huyo anayetuhumiwa kwa mauaji alikuwa anaishi na marehemu nyumba moja baada ya mume wa marehemu ambaye ni mwenyekiti wa mtaa wa National housing Manispaa ya Bukoba David Dominick kumuonea huruma na kumchukua  kuishi naye kama mwanafamilia akifanya shughuli za ujenzi akishirikiana na mwenyekiti tangu mwezi 11,2022. 

Amesema tukio la mauji lilitokea  Februari 13,2023 majira ya saa 12:00 jioni ambapo mtuhumiwa alimpiga marehemu kwa kutumia kitu butu kichwani upande wa kushoto na kumsababishia jeraha kubwa lililopelekea kuvuja damu nyingi na kusababisha kifo chake papo hapo na kisha kumbaka na baada ya kutekeleza tukio hilo aliondoka na kuelekea kusikojulikana.

No comments