HEADER AD

HEADER AD

IFAD, MAWAZIRI WA TANZANIA WAKUTANA KUJADILI MAENDELEO YA UVUVI


Na Mwandishi Wetu, Italia

MKUTANO wa Mfuko wa Maendeleo wa Kilimo na Uvuvi Duniani (IFAD) ulioanza February, 13,2023 umehudhuliwa na Rais wa Mfuko huo, Alvaro Lario pamoja na Mawaziri wa Uvuvi kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), ambapo wamejadili mambo mbalimbali juu ya sekta ya uvuvi.

Viongozi waliohudhulia katika mkutano huo ni pamoja na Mawaziri wawili wa Uvuvi na Makatibu Wakuu wawili, wakiongozwa na Waziri wa Uvuvi Mashimba Ndaki sambamba na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Balozi Mahmmoud Thabiti Kombo ambaye pia ni Mwakilishi wa kudumu wa mfuko huo wa IFAD akiwakilisha Tanzania.

Miradi inayojadiliwa ni pamoja na miradi ya ujenzi wa meli za uvuvi, ujenzi wa masoko, majokofu ya baridi ya kuhifadhi samaki na mazao ya baharini ikiwemo mwani.

Wengine waliohudhuria mkutano huo ambao unatarajiwa kuhitimishwa Februari 16,2023, ni  moja na timu ya maafisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Italia wakiongozwa na Mwambata wa Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Misitu, Jaquiline Mhando.




No comments