HEADER AD

HEADER AD

MADIWANI MUSOMA WAPITISHA BAJETI YA BILIONI 30

 


Na Jovina Massano, Musoma

MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma Mkoani Mara wamepitisha makisio ya kiasi cha Tsh 30,770,982,247.44 katika rasimu ya mapendekezo ya mpango wa bajeti ya halmashauri ya mwaka wa fedha 2023/2024.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Samwel Masika akiwasilisha mpango wa bajeti kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bosco Ndungulu, amesema mapendekezo hayo yanajumuisha bajeti ya mapato na matumizi katika maeneo ya mishahara, matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo.

                    Madiwani

Amesema kiasi hicho cha fedha kinatarajiwa kukusanywa kupitia vyanzo mbalimbali ambapo mapato ya ndani ni Tsh. 4,095,882,489.14 sawa na asilimia 13.3, Luzuku ya matumizi mengineyo kutoka serikali kuu ni Tsh.721,423,000.00 sawa na asilimia 2.3.

Ameongeza kuwa mishahara ni Tsh.18,631,235,258.30 sawa na asilimia 60.5 na miradi ya maendeleo toka Serikali kuu na wadau wa maendeleo ni Tsh 7,322,441,500.00 sawa na asilimia 23.8.

Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo William Gumbo amesema kuwa mpango huu wa rasimu umekidhi mahitaji katika nyanja zote muhumu.

         Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma William Gumbo.

Nae Diwani wa viti maalum Kata ya Mwisenge kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM) Amina Masisa amesema mapendekezo ya rasimu yana vipaumbele katika maeneo muhumu ndani ya jamii yetu.

Ameainisha vipaumbele hivyo kuwa  ni pamoja na uboreshaji wa miundombinu katika elimu ya msingi na sekondari ikiwemo vyoo na maeneo ya kujifunzia na kufundishia, kuongeza miundombinu kwenye vituo vya afya.

      Amina Masisa Diwani wa viti maalum Kata ya Mwisenge.

Amesema lengo ni kuongeza ufanisi wa huduma, kulipa fidia kwa wananchi kwa maeneo yaliyochukuliwa na halmashauri, ukamilishaji wa miradi viporo na kuimarisha ukusanyaji wa mapato pamoja na kubuni vyanzo vipya.

                          Madiwani

           

No comments