HEADER AD

HEADER AD

JOYCE MANG'O : WANANCHI TUMUUNGE MKONO RAIS SAMIA


Na Jovina Massano, Serengeti

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)Bara wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Joyce Mang'o  amewaomba wananchi wilaya ya Serengeti mkoani Mara kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan za uletaji wa maendeleo katika nyanja mbalimbali. 

Akizumgumza hivi karibuni katika mkutano wa hadhara katika maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM kwa jumuia za Chama kimkoa uliofanyika stendi ya zamani wilayani hapo Joyce amewaeleza wananchi  kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Samia imetoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Wilaya hiyo.

      MJumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)Bara wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Joyce Mang'o.

"Tunajionea wenyewe maboresho katika sekta ya elimu ujenzi wa vyumba vya madarasa vinajengwa nchi nzima bila michango ya wananchi, elimu bure, maboresho hayo yameenda hadi kwenye sekta ya afya, miundombinu ya maji, barabara, viwanja vya Ndege, reli hadi kwenye nishati.

Pia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan hakuishia hapo ameimarisha Demokrasia hapa nchini hakika tunajivunia utekelezaji wake, mwenye macho haambiwi tazama anaona mwenyewe hakika wanawake tunaweza"amesema Joyce.

        Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akionesha Ilani ya CCM.

Ameongeza "Wilayani hapa zimetolewa Tsh. Milioni 850, upande wa afya ambapo Tsh.Milioni 750 zimeelekezwa hospitali ya wilaya na Tsh. Milioni 100 zitapelekwa katika vituo vingine vya afya kuhakikisha huduma zinakuwa bora". amesema Joyce.

Naye Diwani wa viti maalum Kata ya Mwisenge kupitia CCM Amina Shabani Masisa amesema kuwa watu wanafikiri na kusema kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM)hakijafanya kitu ni kauli tu za wasioelewa kwani mabadiliko yapo mengi tangu uhuru yanaonekana na Ilani ya CCM inatekelezwa kwa kasi.

          Amina Masisa Diwani wa viti maalum Kata ya Mwisenge Manispaa ya Musoma mkoani Mara.

"Tunatembea kifua mbele miaka 46 ya CCM imefanya mabadiliko makubwa katika nchi yetu miundombinu safi, ongezeko la ajira sekta zote usimamiaji wa sera yetu ya kuhakikisha amani katika nchi yetu na mshikamano kwa wote vinadumu.

"Tunamshukuru pia Rais kuiishi misingi ya Chama na kuhakikisha nchi inasonga mbele na maendeleo yanaendelea kwa Wananchi ", amesema Amina.

Selina Kisiri mkazi wa mnada mpya Burunga wilayani Serengeti ameipongeza Serikali kwa jitihada zake zinazoleta maendeleo kwa wananchi katika mambo mbalimbali.

       Selina Kisiri mkazi wa mnada mpya Burunga.

"Naipongeza Serikali inatuletea maendeleo kwetu ya kutujengea hospitali ninaomba pia waendelee kututengenezea barabara za mitaani nyingi zimeharibika hapa kwetu watuangalie"amesema Selina.

Mjumbe  huyo akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Mara Patrick Chandi, walitembelea kituo cha nyumba salama  na hospital ya wilaya na kupanda miti na kutoa mahitaji ya usafi wodi ya akina mama.

 

      Kulia ni Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Mara Nansi Msafiri akipeana mkono na MNEC Joyce Mang'o.



No comments